Ubongo
 Learning ambalo ni shirika linaloongoza barani Afrika kwa maudhui ya 
elimu ya kuburudisha kwa watoto, leo imeandaa mkutano wake wa mwaka 
ambao ulikuwa na lengo ya kuzungumzia uwezeshwaji kiuchumi, haswa kwa 
wasichana ambao wanaweza kuathirika zaidi ya wavulana  kutokana na 
mabadiliko katika soko la ajira. 
Kwa kipindi cha miezi 6 sasa, Ubongo Learning, shirika lisilo la kibiashara ambalo ndiyo lilibuni katuni za kuelimisha za Ubongo Kids, limekuwa likifanya utafiti juu ya uwezo wa kupata ajira na usimamizi wa fedha miongoni mwa vijana nchini Tanzania.

Lengo
 la mradi huu, uliofadhiliwa na Data for Local Impact (DLI), ni 
kuelimisha vijana, haswa wasichana jinsi ya kutumia maelezo, taarifa na 
takwimu zinazopatikana ili kufanya maamuzi bora juu ya maisha yao ya 
mbeleni, na zaidi ya hilo kupitia ujuzi wa masala ya kifedha. Vipindi 
vya televisheni vya Ubongo vinatazamwa na zaidi ya watu milioni 6.4 kila
 mwezi, hivyo kuvifanya kuwa vipindi vya watoto vyenye watazamaji wengi 
kuliko vyote Afrika Mashariki na kuwa sehemu nzuri sana kuwasilisha 
maswala muhimu kwa vijana. 
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano huo, Meneja Masoko Ubongo Learning Iman Lipumba alisema licha ya kuwa na Maendeleo makubwa ya kuhakikisha wasichana wanaandikishwa shule za msingi, lakini bado jamii nyingi nchini Tanzania bado zinawapendelea wavulana kielimu (hususan kwenye elimu ya shule za sekondari na vyuo vikuu) zaidi ya wasichana.

 Zaidi
 ya hilo, utafiti wetu unaonyesha kuwa wavulana wanashawishiwa zaidi 
kusoma masomo ya sayansi, hesabu na ukandarasi, taaluma ambazo 
zinahitajika sana katika soko la ajira, na wasichana wanashauriwa 
kuingia kwenye masomo ya sanaa na hatimaye kufanya kazi za utoa huduma 
ambazo huenda zikapotea katika miaka michache ijayo. 
 Mwakilishi
wa Catholic Relief Service,Priyanka Jagtap, akiwasilisha mada katika mkutano wa
mwaka wa Shirika lilisilo la Kiserikali la Ubongo Learning linalojishughulisha
na elimu ya kuburudisha watoto. Mkutano huo ulikuwa na lengo ya kuzungumzia uwezeshwaji
kiuchumi, haswa kwa wasichana ambao wanaweza kuathirika zaidi ya wavulana  kutokana na mabadiliko katika soko la ajira
leo jijini Dar es Salaam
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika
lilisilo la Kiserikali la Ubongo Learning linalojishughulisha na elimu ya
kuburudisha watoto, Nisha Lagon, akiwasilisha mada katika  mkutano wake wa
mwaka ambao ulikuwa na lengo ya kuzungumzia uwezeshwaji
kiuchumi, haswa kwa wasichana ambao wanaweza kuathirika zaidi ya wavulana  kutokana na mabadiliko katika soko la ajira
leo jijini Dar es Salaam.Kulia
ni Mwakilishi wa Catholic Relief Service,Priyanka Jagtap.
Mwakilishi
wa BBC Media Action ,Doreen Bangapi,akichangia mada katika katika mkutano wa
mwaka wa wadau wa mwaka wa Shirika lilisilo la Kiserikali la Ubongo Learning
linalojishughulisha na elimu ya kuburudisha watoto. Mkutano huo ulikuwa na lengo ya kuzungumzia uwezeshwaji
kiuchumi, haswa kwa wasichana ambao wanaweza kuathirika zaidi ya wavulana  kutokana na mabadiliko katika soko la ajira
leo jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...