Na Agness Francis,Blogu ya Jamii.

UONGOZI na Kamati ya Maandalizi Klabu ya Yanga SC wamefanya mabadiliko kwa kusogeza mbele tarehe ya Mkutano Mkuu wao.

Mkutano Mkuu wa klabu hiyo ulikuwa ufanyike Mei 5 mwaka huu lakini sasa unatarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu katika Bwalo la Polisi Oyestabey jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Charles Boniphase Mkwasa amesema kamati imekaa na kujadiliana, hivyo wameona wasogeze mbele tarehe ya mkutano huo kwa sababu za kimsingi zilizojitokeza.

"Tuna mechi nyingi za Ligi zitakazokuwa zinaendelea  hapa katikati pamoja na hilo baadhi ya  viongozi watakuwa nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza katika hatua ya makundi katika Shirikisho Barani Afrika dhidi ya  USM Alger, "amesema Mkwasa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makundi ya WhatsApp ya Yanga Tanzania Bakili Makele amewataka wanachama wote wa klabu hiyo nchini kulipi kadi zao.
"Ni muhimu kwa kila mwanachama kulipia kadi yake ya uanachama iwe ya Benki au ya kawaida ili auhudhurie mkutano huo ili kila mmoja apate haki yake ya kuchangia  na hatimaye kuondoa changamoto zilizopo na tusonge mbele,”amesema Makele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...