Na Rhoda Ezekiel Kigoma.
WANAHABARI mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuongeza ubunifu katika kazi zao ili kuchochea maendeleo ya mkoa huo.
Rai hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo amesema uandishi wa habari za matukio umepitwa na wakati kama waandishi wenye taaaluma wanatakiwa kutumia kalamu zao kuandika habari zenye ubunifu na weledi mkubwa kwa kutafuta undani wa habari wanazo ziandika.
Aidha amewataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuwashawishi vijana wadogo kuipenda fani ya uandishi wa habari, kwa kuwatembelea wanafunzi shuleni na kutoa elimu kuhusu fani hiyo ili kuepukana na fani hiyo kuonekana wanaoingia huko ni wale wanaoshindwa kutimiza ndoto zao kwakuwa fani hiyo ni sawa na Fani zingine.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoani wa Kigoma (KGPC)Adela Madyane amesema chama cha waandishi wa habari kina mpango wa kuwaunganisha waandishi wa habari wote mkoani Kigoma ili kuhakikisha wanakuwa na maadili na kuzingatia misingi ya uandishi wa habari.
Amesema Chama hicho kinaendelea kusimamia misingi na taratibu za kitaaluma zilizowekwa kisheria ilikuondoa migogoro baina ya Wanahabari na wadau wa maendeleo, na wanachama wenye vigezo ili kuepuka waandishi wasio na taaluma .
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waandishi wa habari mkoani wa Kigoma.
Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma Fadhili Abdallah amesema kama waandishi wa habari watahakikisha wanashirikiana na wananchi na viongozi kuhakikisha wanaripoti habari zenye tija na maendeleo kwa ajili ya kuuinua mkoa wa Kigoma.
Amesema changamoto wanazokutana nazo kama Waandishi wa habari ni pamoja na baadhi ya viongozi na wadau kuzuia baadhi ya taarifa na kuwanyima ushirikiano Waaandishi pindi wanapo hitaji taarifa na kuomba Viongozi wote kutoa ushirikiano kwakuwa Waandishi wa habari wana mchango Mkubwa wa Kuinua maendeleo hasa katika mikoa ambayo bado iko nyuma.
Pica ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...