Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Suma JKT kuhakikisha madarasa yaliyojengwa katika shule ya Sekondari ya Hombolo Jijini Dodoma yanawekewa madawati kwa gharama ya shilingi milioni 20 .

Ameyasema hayo wakati alipokagua shule hiyo leo kuona maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne yaliyojengwa kwa kutumia “FORCE ACCOUNT “ambapo alibaini uduni mkubwa katika ujenzi wa madarasa hayo.

Mhe. Jafo amesema inashangaza kuona maeneo mengine wametumia fedha zilizotolewa na Serikali kujenga madarasa pamoja na kuweka madarasa tofauti na Jiji la Dodoma hivyo ameagiza kuhakikisha wanatumia fedha zilizobaki milioni 20 kwa ajili ya kuweka madawati.“Naagiza, uongozi wa Jiji la Dodoma na SUMA JKT kuhakikisha madarasa yote manne yaliyojengwa kwa fedha za Serikali yamewekwa madawati kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia na kuwa na mazingira mazuri ya kuapata elimu.” Anasema jafo

Mhe. Jafo amefafanua kuwa SUMA JKT wameenda kinyume na matakwa ya Serikali ya kujenga madarasa na kuweka maruru kitendo ambacho kinarudisha nyuma uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kurudisha maendeleo katika jiji la Dodoma.Mhe. Jafo amesema kuwa amekerwa na uhafifu wa zege lililotumika katika ujenzi wa sakafu ya madarasa hayo ambapo mpaka sasa yameanza kuvunjika kabla ya kutumika.Aidha amewataka kurekebisha sakafu hiyo mapema.

“Ninawaagisa kuvunja sakafu ya madarasa na kujenga nyingine, na msinipe mashaka na kuanza kukagua ubora wa majengo yaliyojengwa na kukuta yako chini ya kiwango, nataka madarasa ambayo sakafu yake ni imara na ya kudumu” amesema Jafo.Akifafanua kuhusu matatizo ya maji Mhe. Jafo amesema Serikali imejipanga kutatua kero ya maji nchini na itachimba kisima kitakachotoa maji kwa shule hiyo.

Aidha amewaka wanafuzi hao kunzingatia masomo kwa kusoma kwa bidii na kuwa na kampeni maalum ya kuondoa ziro ili kuondokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne na cha Sita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa maagizo kwa Mkandarasi SUMA JKT baada ya kukagua ujenzi wa madarasa manne LEO yaliyojengwa katika shule ya Sekondari ya Hombolo, Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akikagua ujenzi wa sakafu wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Hombolo, Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Hombolo leo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne katika shule hiyo. 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Hombolo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo alipotembelea shule hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...