Na Jumia Food Tanzania

Kikiwa kimeanzishwa takribani miaka 10 iliyopita, kituo cha kulea watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kinakumbwa na changamoto kadhaa zikiwemo eneo la kutosha kuwalea na kuwahifadhi watoto pamoja na bima ya afya.
Kituo hiki ambacho mpaka hivi sasa kina jumla ya watoto 48 wakiwemo wavulana 26 huku 22 ni wasichana. Watoto hao wanaolelewa na Bi. Zainab Bakari ambaye ndiye mwanzilishi na mlezi wa watoto hao, anawahudumia kwa mahitaji yao yote muhimu yakiwemo malazi, chakula, mavazi, shule, afya na mengineyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile serikali, sekta na watu binafsi kupitia misaada inayopelekwa kituoni hapo.

Akizungumza wakati akipokea msaada wa chakula na mahitaji ya shule kutoka kampuni ya Jumia Food, Bi. Bakari ameelezea kuwa watoto wanazidi kuongezeka kituoni kwake hali inayopelekea kuwa ni changamoto kuwahifadhi na kuwalea katika eneo moja kama inavyotakiwa.
“Kituo hiki nilikianzisha takribani miaka 10 iliyopita nikiwa na watoto wachache hapa kwenye hii nyumba yetu. Na kwa kipindi chote hiko nimekuwa nikipokea watoto na kuwalea hapahapa. Hivyo, kadri miaka inavyozidi kwenda ndivyo ninavyozidi kupokea watoto, wakizidi kukua na mahitaji kuongezeka.

 Hali hiyo imepelekea suala la kuwalea wote kwa pamoja kuwa ni changamoto kwasababu kituo hiki hakina uzio na kimezungukwa na nyumba za watu wengine,” alielezea Mwanzilishi na Mlezi wa Kituo cha Maunga.

Jumia Food, kampuni inayojihusisha na huduma ya chakula kwa njia ya mtandao ilikuwa ikiendesha kampeni iliyokwenda kwa jina la “STAND BY ME” katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kampeni hii iliwashirikisha wateja wake kwa kuwataka kuagiza chakula kwa kutumia nenosiri ‘ASANTE’ ili kuchangia mahitaji ya chakula kituoni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...