Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
HALMASHAURI ya wilaya ya Bagamoyo ,Pwani inakabiliwa na upungufu mkubwa wa miundombinu katika sekta ya elimu ikiwemo vyumba vya madarasa 367 ambapo shule za msingi kuna upungufu 329 huku shule za sekondari upungufu ni 38. Aidha kuna upungufu wa matundu ya vyoo 770 huku nyumba za walimu zipo pungufu 634.
Akitoa taarifa ya masuala ya elimu katika maadhimisho ya Juma la elimu wilayani Bagamoyo ,kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo, ofisa elimu msingi ,Peter Fussi alisema upungufu huo unasababisha kero ya mlundikano wa wanafunzi madarasani. Alisema ,shule za msingi zina mahitaji ya madarasa 621 ,yaliyopo 292 na mapungufu ni 329.
Alitaja mahitaji ya matundu ya vyoo kuwa ni 1,133, yaliyopo 363 ,upungufu 770 ,nyumba za walimu mahitaji 707, zilizopo 73 upungufu 634, maktaba 32 ,zilizopo 25 na pungufu saba. Kwa mujibu wa ofisa elimu msingi huyo ,kwa upande wa elimu msingi wanaendelea na jitihada kwa kushirikiana na wananchi na wadau kujenga vyumba vya madarasa 74 katika kata mbalimbali. Fussi alisema, pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali na wadau bado upo upungufu huo.
"Kwa upande wa elimu sekondari ,alisema ipo miradi inayotekelezwa ni ujenzi ikiwemo ujenzi wa madarasa manne shule mpya ya sekondari Mapinga. Miradi mingine ni umaliziaji wa ujenzi wa maabara mbili shule ya sekondari Kingani ,ujenzi wa nyumba mbili ,ofisi shule ya sekondari Hassanal Damji ,bweni shule ya sekondari Dunda na jengo la utawala shule ya sekondari Kerege" alisema.
Fussi alisema kukamilika na kutumika kwa miradi hiyo kutasaidia kuboresha mazingira ya kusomea na kufundishia kuwa bora na hivyo kuongeza ufaulu wa wanafunzi. Hata hivyo ,alielezea wananchi kupitia madiwani wameelimika vya kutosha ambapo kila kata ina mpango kazi wake wa ujenzi wa miundombinu yake ya elimu na huduma nyingine za jamii.
Pamoja na hayo alisema kuwa limekuwepo tatizo kwa baadhi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na wale wanaojiunga na kidato cha kwanza kutokujua kusoma,kuandika na kuhesabu (KKK).Fussi alibainisha ,tafiti zinaonyesha upo ukweli wa jambo hilo ,linalosababishwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi unatokana na upungufu wa madarasa.
Alisema wapo walimu wasio na mafunzo ya KKK ambao kutokana na upungufu wa walimu wanapewa kufundisha madarasa ya chini yenye kuhitaji walimu wenye mafunzo na waliobobea katika utumiaji wa mbinu na zana za KKK.
Akizungumzia suala la mdondoko ,Fussi alisema idadi ya wanafunzi wanaokatisha masomo kwasababu mbalimbali( mdondoko) imepungua.Alisema kuwa mwaka 2016/2017 katika shule za msingi kulikuwa na mdondoko 23 na shule za sekondari utoro 29,mimba 7 jumla mdondoko 43.
Aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Bw. Alphonce Amuli  aliwataka wananchi kushirikiana na walimu kuangalia namna ya kutatua changamoto za miundombinu na kuinua ufaulu mashuleni. Alisema serikali ama walimu pekee hawawezi kupambana na changamoto hizo hivyo kuna kila sababu ya kuungana pamoja kumaliza kero hizo.
 Mgeni rasmi Bw. Alphonce Amuli akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu wilayani humo yaliyofanyika shule ya msingi Majengo.


Ofisa elimu ya msingi halmashauri ya Bagamoyo Bw. Peter Fussi akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Fatuma Latu wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu kiwilaya iliyofanyika shule ya msingi Majengo. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...