Sisi familia tunatoa shukrani za pekee kwa Mungu kwa jinsi alivyoweza kutulinda na kutupa faraja ya pekee katika kipindi chote cha majonzi na hadi sasa unatimiza mwaka bila kuwa nawe. Tunakukumbuka sana mama yetu japo kimwili haupo nasi pengo lako daima haliwezi kuzibika. 

Tunakumbuka upendo wako, ushauri wako, upole na ucheshi wako pamoja na ukarimu wako ambao ulimfanyia kila aliyekufahamu kuguswa kipekee.  Kipekee unakumbukwa sana na mumeo  Mzee Vincent William Semkuruto watoto wako Naomi, Jane, Caroline, Samweli, Dolly, Diana pamoja na wajukuu wako, ndugu,  jamaa na marafiki.

‘Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda, nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana atanipa siku ile.” 2 Timotheo 4:7-8              
Pumzika kwa Amani Mama    
Amen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...