Sisi familia tunatoa shukrani za pekee kwa Mungu kwa jinsi alivyoweza kutulinda na kutupa faraja ya pekee katika kipindi chote cha majonzi na hadi sasa unatimiza mwaka bila kuwa nawe. Tunakukumbuka sana mama yetu japo kimwili haupo nasi pengo lako daima haliwezi kuzibika.
Tunakumbuka upendo wako, ushauri wako, upole na ucheshi wako pamoja na ukarimu wako ambao ulimfanyia kila aliyekufahamu kuguswa kipekee. Kipekee unakumbukwa sana na mumeo Mzee Vincent William Semkuruto watoto wako Naomi, Jane, Caroline, Samweli, Dolly, Diana pamoja na wajukuu wako, ndugu, jamaa na marafiki.
‘Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda, nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana atanipa siku ile.” 2 Timotheo 4:7-8
Pumzika kwa Amani Mama
Amen



Miss you mama, RIP
ReplyDeleteRIP Mama
ReplyDeleteYou will be missed Bibi RIP.
ReplyDelete