*Azindua kitabu cha Mafunzo ya umeme wa jua 
*Atashauri kisambazwe kwa wataalam ,mafundi mitambo 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa amewataka watalaam wote na taasisi zinazohusika na nishati ya umeme-jua kuangalia namna ya kupanua wigo wa matumizi ya nishati hiyo ya jua ambayo ipo kwa wingi katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania. 

Amefafanua katika kiwango cha Gigawatt 400 za umeme jua zinazotumika duniani kwa sasa bado ni Gigawatt moja tu ndio zimefungwa na kutumika katika nchi za Afrika ,Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa namna mbili. 

Mkapa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua Kitabu cha Mafunzo ya Umeme wa Jua ambacho mtunzi na mwandishi wake ni Godwin Msigwa.Kitabu hicho ambacho kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili kitasaidia kusambaza taaluma na maarifa katika eneo la nishati ya umeme wa jua nchini. 

Akizungumza kabla ya kuzindua kitabu hicho ambacho ameomba kisambazwe kwa watalaamu wa nishati ya umeme jua na mafundi mitambo wa umeme jua, amesema pamoja na duniani kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme unaotokana na jua bado nchi za Afrika zipo chini kwenye matumizi. 

Mkapa amefafanua kwa mujibu wa taarifa za Mtandao wa jarida la kimataifa la nishati Jadidifu linaloitwa REN 21 ya 2018 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2017 jumla ya zaidi ya Gigawatt 400 za umeme jua zimefungwa duniani kote kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme ambayo sote tunaifahamu kuwa ni nishati muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Aidha amesema ongezeko la uzalishaji wa umeme duniani kote linatokana na uzalishaji kwa kutumia umeme-jua lilifikia Gigawatt 380 katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2017. "Ongezeko hilo ni la kasi sana, jambo ambalo linaashiria kuwa kuna mwelekezo mkubwa duniani wa matumizi ya nishati ya umeme unaozalishwa kwa kutumia nishati ya jua. 
Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza katika uzinduzi wa Kitabu cha Mafunzo ya Umeme Jua Kilichoandikwa na Godwin Msigwa katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijini Dar es Salaam.
.Mwenyekiti wa Bodi ya Costech, Profesa Makenya Maboko akitoa shukrani kwa Mgeni Rasmi Benjamin Mkapa.
Rais wa Awamu ya Tatu akitoa kitabu baada ya kukata utepe.
Rais wa Awamu ya Tatu akitoa kitabu baada ya kukata utepe.
Mtunzi wa Kitabu cha Mafunzo ya Umeme Jua, Godwin Msigwa akieleza malengo ya kitabu hicho na hatua alizozipitia, hafla ilifanyika katika ukumbi wa Costech kijiji Dar es Salaam.

Baadhi ya Wadau waliohudhuria hafla hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...