Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

*Asisitiza umuhimu wa kumuombea Rais Magufuli ili atekeleze yale anayoyafanya kwa maslahi ya Taifa

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesisitiza umuhimu wa Watanzania kudumisha umoja, amani na mshikamano huku akitoa rai ya kuendelea kumuombea Rais Dk. John Magufuli ili aendelee kulitumikia Taifa. 

Alhaj Mwinyi ametoa kauli hiyo leo mbele ya mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kumalizika kwa ibada ya swala ya Eid ambayo kitaifa ilifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dr es Salaam. "Niwaombe ndugu zangu na watanzania wote tuendelee kudumisha umoja na mshikamano.

"Tuvumiliane kwa kila jambo na kubwa zaidi tuhakikishe tunaendelea kuitunza amani yetu ili tubaki kuwa salama,"amesema Alhaj Mwinyi. Aidha amewaomba Watanzania kuhakikisha wanaendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli ili aendelee kuwatumikia Watanzania hasa katika kuleta maendeleo. Amefafanua kuna mambo ambayo Rais Magufuli amekuwa akiyafanya kwa maslahi ya chini, hivyo ni kujukumu la kila mwananchi kuombea mwa Mwenyezi Mungu aendelee kuyafanikisha yote aliyoyaanzisha. 

Awali Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akizungumza na waumini waliokuwa kwenye viwanja hivyo amehimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuzingatia mafunzo ambayo wameyapata wakati wa mfungo wa Ramadhan. Pia amehimiza Watanzania kuendelea kudumisha umoja na mshikamano huku akielezea umuhimu wa kushirikiana.

Ametumia nafasi hiyo kuzungumzia Hijja ambapo amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA)limeanza kupokea waumini wa dini ya Kiislamu ambao wanataka kwenda Hijja mwaka huu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...