Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MICHUANO ya Kombe la Dunia imeendelea tena leo nchini Urusi huku Timu ya Taifa England ikiishushia kichapo Timu ya Taifa ya Panama mabao 6-1 huku Senegela na Japan wakitoka sare ya 2-2.

Kwa upande wa ushindi ambao England wameupata tayari wamejihakikishia kuingia hatua ya pili wakati Panama sasa kwa matokeo hayo wanalazimika kuondoka kwenye michuano hiyo.

Mechi kati ya England na Panama kwa sehemu kubwa ilitawaliwa na akili nyingi za kisoka na hasa kwa wachezaji wa England walionesha kuutawala mchezo huo.Pasi maridadi na zenye uhakika ambazo zilikuwa zinapigwa na wachezaji wa England zilisababisha Panama kupoteza muelekeo na mvua ya magoli ikaanza.

Mabao matatu ya England yamefungwa na mshambuliaji Harry Kane aliyekuwa nyota wa mchezo huo.Wafungaji wengine ni John Stones ambaye yeye alipachika mabao mawili na mshambuliaji Jesse Lingard akitupia goli moja.Hata hivyo Panama ambao licha ya kufungwa mabao hayo mashabiki wake walionekana wenye furaha na wanaoshangilia bila kuchoka na ilipofika dakika ya 78 ya mchezo timu yao ikapata bao moja lililofungwa na Felipe Baloy.

Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika England wameibuka na ushindi huo mnono.Kwa matokeo hayo England wanashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na alama sita na Ubelgiji inashika nafasi ya pili kwa alama sita na tofauti iliyopo ni idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.


SENEGAL , JAPAN WATOA SARE YA 2-2

Mchezo mwingine kwenye michuano hiyo ni kati ya Senegal na Japan ambapo hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2.
Mechi kati ya Senegal na Japan zilikuwa zinasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soko hasa wa Bara la Afrika kutokana na kuipa nafasi Senegal kutokana na ushindi walioupata kwenye mchezo wao wa kwanza.

Ushindi wa Senegal katika mchezo wa kwanza uliibua shangwe kwa mashabiki wa soko wa Afrika wakiamini huenda ikafika mbali.Katika mchezo wa leo Senegal ilikuwa ya kwanza kupata bao kwani katika dakika ya 11 mshambuliaji wake Sadio Mane aliandika bao la kuongoza.

Hata hivyo mpira huo ulikuwa na kasi na ushindani wa hali ya juu kutokana na kila timu kuonesha umahiri hasa katika kusakata kabumbu ambapo nguvu, akili, mbinu za mchezo na pasi zilisababisha mechi kuwa na mvuto wa aina yake.Dakika ya 34 ya mchezo Japan wakasawazisha kupitia kwa mchezaji wake Takashi Inui.Kasi ya mpira iliendelea na ilipofika dakika ya 71 Mshambuliaji wa Senegal Moussa Wague akaipatia timu yake bao la pili.

Bao la pili la Senegal lilidumu kwa dakika nane tu kwani ilipofika dakika ya 78 Japan wakapata bao la kusawazisha baada ya mchezaji wake Keisuke Honda kupata bao.Hivyo hadi mpira unamalizika mabao yalikuwa 2-2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...