Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .
Taasisi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo nchini (PASS) imeingia makubaliano na Mfuko wa uwekezaji wa biashara na kilimo Afrika (AATIF) kusaidia wadau wa sekta ya Kilimo nchini kwa kutoa mikopo mikubwa itakayowezesha utekelezwaji wa miradi mikubwa ya kilimo.
Makubaliano haya baina ya PASS na AATIF yanatajwa kuwa mkombozi wa changamoto za muda mrefu za wadau wa sekta ya Kilimo ambao wamekuwa wakipitia kwa kushindwa kupata mikopo ya muda mrefu kutoka kwa taasisi za kifedha hapa nchini kutokana na ufinyu wa muda wa urejeshwaji wa mikopo hiyo.
Kwa kiasi kikubwa hali hii imekuwa ikitajwa kama sababu ya sekta hii kushindwa kuwa na maendeleo makubwa kutokana na mipango mingi kujikita katika uwekezaji wa muda mfupi.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutambulisha fursa hiyo kwa wadau wa kilimo na baadhi ya taasisi za fedha iliyofanyika mapema leo asubuhi katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Bwana Nicomed Bohay amesema.hatua ya upatikanaji wa mikopo mikubwa na ya muda mrefu kwa wadau wakubwa wa kilimo utachochea ukuaji wa sekta ya kilimo.
“Malengo yetu sisi ni kutengeneza mashirikiano baina ya taasisi hizi ili ziweze kupata mikopo hii, imani yetu kama PASS nikuwa itachochea uwekezaji mkubwa katika maeneo mbalimbali ya kilimo na hivyo kuifanya sekta ya kilimo nchini kuwa mdau mkubwa wa falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya kuziwezesha sekta binafsi na hasa kilimo katika kushiriki katika uchumi wa viwanda” Amesema Bwana Nicomed Bohay.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...