Watoto kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali mapema jana katika kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Elimu bure inatakiwa iende sambamba na huduma muhimu kwa watoto ikiwemo upatikanaji wa maji, vyoo vya kutosha, vyumba vya kujihifadhia watoto wa kike, Mabweni pamoja na chakula kwa wanafunzi wawapo mashuleni.

Hayo yamesemwa mapema jana jijjini Dar es salaam na Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Anna Sangai katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ifikapo tarehe 16 mwezi juni.
Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Anna Sangai akiongea na waandishi wa habari baada ya maandamano ya amani yaliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam.

Afisa huyo alisema kuwa lengo kuu la kukutana pamoja na watoto hao ni kutathmini sera na mipango ya nchi iliyowekwa katika kulinda, kutetea haki na maslahi ya mtoto kulingana na sharia na mikataba ya kimataifa ambayo taifa letu limeingia.

Aliendelea kusisitiza kuwa jambo hili liende sambamba na ulinzi wa watoto wawapo ndani na nje shule, lakini pia kuwalinda dhidi ya mila na desturi zinazowakandamiza watoto hasa wa kike kama vitendo vya ukeketaji, ndoa pamoja na mimba za utotoni.

Lakini pia katika kukuza na kuendeleza uchumi wa viwanda watoto wasiachwe nyuma kwani wao ndio wanaotarajiwa kuja kuviendesha viwanda hivyo tarajiwa katika nchi yetu kwa kuwakuza kwa elimu ya vitendo ikiwemo masomo kilimo.
Mwenyekiti wa vituo vya Taarifa na Maarifa Taifa Janeth Mawinza akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Mwananyamara jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata Makumbusho Dada Janeth Mawinza alisema kuwa wameamua kufanya maadhimisho hayo katika eneno la Mwananyamara Kisiwani kutokana ni eneo ambalo waligundua matukio mengi ya ukatili wa watoto ikiwemo kupigwa kunakopitiliza pamoja na matukio ya watoto kuchomwa moto.

“Eneo la Mwananyamara Kisiwani lina watoto wengi sana waliofanyiwa ukatili na ndio maana tumekuja na ujumbe unaowataka wazazi na walezi kuacha vitendo hivyo mara moja, kwani mtoto ana haki zake na anastahili kulindwa na kuendelezwa ili aweze kufikia malengo yake”. Alisisitiza Dada Mawinza
Watoto kutoka kata mbalimbali wakiwa katika maandamano ya amani Siku ya Mtoto wa Afrika mapema jana jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...