*Ni katika banda lao lililopo Maonesho ya biashara viwanja vya Sabasaba
*Meneja Masoko azungumzia mikakati yao kuelekea Tanzania ya viwanda

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Cholemu Investment Limited ambayo inajihusisha na uuazaji aridhi ikiwemo viwanja na mashamba imesema kwa kutambua kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda kwa sasa ipo katika mchakato wa kuanza kuuza maeneo yaliyopimwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda nchini .

Hayo yamesmwa leo kwenye Maonesho ya Biashara ya kimataifa ya 42 yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam na Meneja Masoko wa Kampuni ya Cholemu Investment Limited Swaumu Mohamed.

Asema kampuni yao kwa muda mrefu imejikita katika uuzaji wa viwanja kwa gharama nafuu mbayo kila mwenye kuhitaji kiwanja atamudu na kutokana na unafuu wao wa bei idadi kubwa ya wananchi wamenunua viwanja kutoka kwenye kampuni yao.

Amesema pamoja na kukijita katika uuzaji wa viwanja na mashamba wamejijenga sifa kwani kampuni yao uhakikisha aliyenunua kiwanja kutoka kwao anapata hati ya Wizara ya Maendeleo ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

“Tupo mbioni kuanza mchakato wa kuanza kuuza na maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.Ni wajibu wetu kama kampuni ya kizalendo kuhakikisha tunaunga mkono kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda.

"Hivyo tumeamua kuunga mkono kwa vitendo kwa kuanza mchakato wa kuuza maeneo ambayo yatatumika kwa ujenzi waviwanda,”amesema.Mohamed.

Amesema kwa kuwa wanayo miradi mingi ambayo wanaendelea kuipima kwa ajili ya viwanja wanaangalia namna ya kupima na maeneo maalumu kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

Kuhusu uwepo wao kwenye maonesho hayo amesema kikubwa wanataka kuwaambia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla shughuli ambazo kampuni yao inafanya katika uuzaji wa ardhi.

Akizungumzia baadhi ya maeneo ambayo wanayo kwa ajili ya viwanja ni Kigamboni, Bagamoyo, Kibaha, Chanika, Morogoro, Mbweni(Kilakala), Mabwe Pande, Arusha eneo la Kisongo.

Amewaomba wananchi wanaofika kwenye maonesho hayo kufika kwenye banda lao ili kupata maelezo kuhusu viwanja na bei zake na kubwa zaidi lengo lao ni kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uhakika wa eneo ambalo limepimwa kwa ajili ya makazi.

Idadi kubwa ya wananchi wanaendelea kufika katika banda la Cholemu Investment kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi huku wengine wakichangamkia viwanja hivyo ambavyo gharama yake ni nafuu na mnunuaji analipa fedha kigogo kigogo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Cholemu Investment,Swaumu Mohamed  akizungumza na Globu ya jamii  leo jijini Dar as Salaam juu ya kuuza mashamba,viwanja bila riba wala dhamana yoyote katika
maonyesho ya biashara ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Mendeleo ya Biashara TANTRADE. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...