Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,    Bw. Kagera Ng’weshemi (kushoto) akimueleza mwananchi kuhusiana na uchunguzi wa kimaabara wa dawa za kulevya na sumu unavyofanyika kwa hatua mbalimbali ndani ya maabara za Mamlaka.
 Mmoja ya wananchi akimsikiliza mtumishi wa Mamlaka, Bi. Petronila Foy (kulia) akimuelezea kuhusiana na utaratibu wa kufuata unapohitaji kusajili kemikali kwa ajili ya kutumia, kuuza, kusafirisha au kuingiza nchini.

 Mtumishi wa Mamlaka, Bw. Alois Ngonyani (kushoto) akitoa elimu kuhusu aina za dawa za kulevya na madhara yake kwa wadau waliotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye Maonesho ya Saba Saba yanayoendelea kwenye viwanja vya Saba Saba, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.


Bi. Leticia Waitara (kushoto) akitoa elimu kwa wadau kuhusiana na taratibu za uchunguzi wa Vinasaba vya Binadumu (DNA) na mpaka hatua ya mwisho ya uchunguzi unavyofanyika kwenye Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...