Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema kuwa asilimia 85 ya mazao yanachavishwa na nyuki hivyo wakiondolewa wanaweza kusababisha ukosefu wa chakula duniani.

Profesa Silayo amesema hayo jijini Dar es Salaam wakatiakizungumza katika Siku Maalum ya Asali ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza hatua mbalimbali zinazchukuliwa na TFS katika sekta ya Asali. 

Akifafanua zaidi amesema uchavishwaji wa mazao unafanywa na nyuki kwa asilimia kubwa, hivyo wakiondolewa duniani hakutakuwa na chakula."Kwahiyo watumiaji mnayo fursa ya kuuza nyuki...kuna makundi takribani milioni 10 ya nyuki ambao wamekuwa wakizagaa hovyo, hivyo kupitia fursa hii itatusaidia kuzalisha makundi ya nyuki ambayo yatauzwa sehemu mbalimbali," amesema.

Amesema uuzaji wa asali na nta umeongezeka ambapo mwaka 2012 ziliuzwa tani 137 na kuingiza pato la Sh. Bilioni 1.05 na kwa mwaka 2016 iliuza tani 241 sawa na Sh. Bilioni 2.
Amesema ongezeko hilo limechangiwa na maboresho mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanyika na hivyo katika kuelekea uchumi wa viwanda, sekta ya nyuki ni miongoni kwa sekta inayokuwa kwa kasi sana.

Profesa Silayo amesema mbali na mafaniko hayo kumekuwepo na changamoto nyingi ikiwemo kutokufikiwa kwa wadau mbalimbali ambao wako pembezoni kwa nchi pamoja na ubora wa asali na mazao kutokufikia kiwango cha kimataifa.Akifafanua zaidi kuhusu asali, Profesa Silayo amesema amepata nafasi ya kuzungumza na wadau wa asali nchini na kwamba kwa sehemu kubwa wanahitaji kuendelea kuelimishwa zaidi kuhusu masoko.
Amesema TFS imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha mazingira na kuhamasisha bidhaa ya asali ambapo asali ya Tanzania ina soko kubwa na inapendwa. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(Tantrade), Edwin Rutageruka, Emmanuel Miselya amesema mazao ya asali yamekuwa yakiongezeka nchini ambapo tani 138 zinazalishwa.Amesema wameamua kuweka siku hiyo maalum yenye kauli mbiu ya 'Mazao ya Nyuki kwa Maendeleo ya Viwanda' lengo likiwa kuwapa fursa wadau mbalimbali ili kukutana na kubadilishana mawazo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki.Wakati huohuo wafanyabiashara wa asali nchini wamemetoa ombi la kupata soko la uhakika.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS )  Profesa Dos Santos Silayo akipewa maeezo kuhusiana na bidhaa ya Asali inavyopatikana na changamoto zake katika suala zima la biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...