Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kijiti cha kuiongoza Wizara yake alichokabidhiwa na aliyekua Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba, atakikimbiza kwa kasi kwa kuwa yeye aliwahi kuwa mwanariadha. 
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano yaliyofanyika ofisini kwake, jijini Dodoma leo, Lugola alisema amekabidhiwa kijiti cha majukumu hayo mapya atahakikisha anasonga mbele kwa kutekeleza majukumu aliyopewa na Rais John Magufuli. 
“Leo nimekabidhiwa ofisi, nimekabidhiwa dhana alizokua anatumia Daktari wa Falsafa Mwigulu, pamoja na shughuli alizokua anazifanya mpaka hapa alipofikia, pia mimi niliwahi kuwa mwanariadha, na nilikua nashiriki mbio za kupokezana kijiti, na  unapokabidhiwa kijiti, hautazami nyuma, ni kuendelea na safari,” alisema Lugola. 
Pia Waziri Lugola alisema anapenda kuwaaambia Watanzania kuwa, atafanya kazi kwa kujiamini na yale mambo ambayo alielekezwa na Mheshimiwa Rais Magufuli kuyafanyia kazi, anaahidi atayashughulikia pamoja na majukumu mengine ya kiutendaji. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo. Hata hivyo, Waziri Lugola alisema aliwahi kuwa mwanariadha, hivyo atahakikisha anasonga mbele kuendelea na safari, hata angalia nyuma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akipongeza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba mara baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Katibu wa Waziri Nelson Kaminyoge, alipokua anataka kumkabidhi taarifa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba ilia aweze kukabidhiwa taarifa hizo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisi ya Waziri huyo, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuaga aliyekua Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba, mara baada ya kukabidhiwa taarifa kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...