SHIRIKA la Utangazaji Nchini (TBC) limezindua studio kubwa ya Kumbukumbu ya ukombozi wa Afrika ya Mwalimu Nyerere katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.
Studio hiyo yenye kuhifadhi historia ya kumbukumbu ya ukombozi barani Afrika zilizopo katika kanda za sauti na video imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya TBC na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na wadau wengine wa maendeleo.
Kuwapo kwa studio hiyo kumelenga kuongeza uwajibikaji, uwezo wa kupata taarifa za zamani na kuongeza uratibu wa menejimenti ya hifadhi ya mambo muhimu ambayo ni ya urithi wa Tanzania.Studio hiyo ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa hifadhi ya mambo ya urithi (TAHAP) wenye lengo la kuhamasisha hifadhi na utunzaji wa urithi wa Tanzania na kumbukumbu za mapambano ya ukombozi katika bara la Afrika, pia itaongeza uelewa wa watanzania juu ya urithi wao ambao umekuwa ukiongezeka jinsi miaka inavyozidi kusonga mbele.
Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo na Msemaji Mkuu wa serikali Dk. Hassan Abbas alisema kwamba serikali itaendelea kuhakikisha kwamba urithi wa nchi hii unahifadhiwa kwa manufaa ya kizazi kijacho.
"Kwa sasa tunaondoka katika mfumo wa maandiko, sauti na video. Sisi kama serikali tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba matukio yetu ya kihistoria yanarekodiwa na kuhifadhiwa vyema. Hatua hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa historia kwa watu wetu na serikali kwa ujumla," alisema Dk Abbas .
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari na Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ,Dkt. Hassan
Abbas (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio
za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika
zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini
Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia
mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini. Kulia ni Mkurugenzi
Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Ms.Anna Therese
Ndong-Jatta(kulia) wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika
la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba, Mwakilishi wa Jumuiya ya
Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw. Charlie Stuart na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez.
Mkurugenzi
Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan
Abbas (wapili kulia) akishuhudia Mkurugenzi Mwakilishi mkazi wa Kanda ya
Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Anna Therese Ndong-Jatta (wa pili
kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa
(TBC) Dkt. Ayub Rioba moja ya Kamera pamoja na vifaa mbalilmbali vya
utangazaji vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na wadua na
Washirika wa Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio
za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika
zilizopo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini
Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia
mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya nchini. Kushoto ni Mwakilishi
wa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie
Stuart.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt.
Hassan Abbas (wa pili kulia) akishuhudia Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya
(EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bi. Charlie Stuart akimkabidhi
moja ya kifaa cha kurekodia kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la
Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba kati ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa
msaada na UNESCO kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla
ya uzinduzi wa studio za Mwalimu Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za
Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo katika Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ukarabati wa Studio
hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake unaofadhiliwa na Umoja wa
Ulaya (EU) nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan
Abbas (katikati) akishuhudia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro
Rodriguez akimkabidhi moja ya kifaa cha kuhifadhia kumbukumbu Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba kati ya
vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na UNESCO kwa kushirikiana na
Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Mwalimu
Nyerere-Kumbukumbu ya Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo
katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyofanyika jijini Dar es
Salaam. Ukarabati wa Studio hiyo umefanywa na UNESCO kupitia mradi wake
unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
Kutoka
Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi wa
Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw.Charlie
Stuart, Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa
UNESCO Bi.Anna Therese Ndong-Jatta, ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas, Mkurugenzi
Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba wakiwa
kwenye picha ya pamoja wakati mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya
utangazaji vilivyotolewa msaada na UNESCO Kwa kushirikiana na wadau wa
mradi wa Umoja wa Ulaya.(EU)
Mkurugenzi
Mwakilishi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO Bi. Anna
Therese Ndong-Jatta, (wa tatu kulia) Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU)
kwa Tanzania na Afrika Mashariki, Bw. Charlie Stuart (kushoto), Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP),Bw. Alvaro Rodriguez ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi
Mkuu wa shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayub Rioba,
wakimsikilza kwa makini mmoja wa wafanyakazi wa TBC akiwaonyesha moja ya
mitambo iliyotumika kurekodia enzi kupigania ukombozi wa Afrika.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...