Na Agness Francis, Blogu ya jamii

VIONGOZI wa Klabu Yanga wameamua kukutana na wachezaji Hassan Kessy na Kelvin Yondan kwa ajili ya kuhakikisha wanabaki katika klabu hiyo

Hata hivyo bado haijafahamika iwapo wamemalizana na wachezaji hao au laa zaidi ya kuwa wamewaita na kukutana nao katika Ofisi za Abass Tarimba leo jijini Dar es Salaam .

Hatua hiyo imekuwa wakati kukiwa na madai kuwa kuna uwezekano tayari Yondan ameshafanya mazungumzo na Simba FC na kilichobakia ni kuingizwa fedha tu ili asaini.

Hivy wakati kukiwa na madai hayo viongozi wa Yanga nao inaelezwa wamefanya mazungumzo na wachezaji hao ili waweze kubaki kwenye klabu hiyo kwa ajili ya msimu wa ligi kuu unaotarajia kuanza Agosti 22 mwaka huu.

"Wachezaji hao wameitwa na viongozi wa Yanga kwa ajili ya mazungumzo.Hata hivyo bado hatujafahamu nini ambacho kimeendelea aidha wamekubali kubaki au laa,"amesema mmoja wa watoa taarifa.

Wakati hayo yakiendelea wachezaji ao wamegoma kusafiri na timu kutokana na kutolipwa fedha zoa za usajili wa msimu ujao.

Wachezaji hao walitakiwa kuambatana na wenzao kuelekea nchini Kenya kucheza mchezo wa raundi ya tatu kundi D dhidi Gor Mahia katika katika michuano inayoendelea ya Shirikisho barani Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...