Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika Yanga wameendelea kusalia kwenye nafasi ya mwisho ya Kundi D baada ya kukubali kichapo cha golo 3-2 kutoka kwa Gor Mahia ya Nchini Kenya.

Mchezo huo uliochezwa kuanzia majira ya saa 1 usiku katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ilichukua dakika moja kwa Gor Mahia K'Ogalo kuandika goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake George Odhiambo Ogutu baada ya kumalizia mpira uliotemwa na golikipa Youthe Rostand.

Yanga  wakiwa wanajaribu kutuliza kasi ya Gor Mahia pamoja na kusaka goli la kusawazisha lakini katika dakika ya 41 kupitia kwa mshambuliaji Mnyarwanda Jacques Tuyisenge aliipatia Gor Mahia golo la pili kwa shuti la mbali baada ya kuanzishiwa mpira na kiungo Mkenya, Francis Kahata mpira wa adhabu ndogo.

Katika mchez uliochezeshwa na marefa kutoka Mauritius Ahmad Imtehaz Heeralall aliyepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera Cauvelet Louis Ralph Fabien na Akhtar Nawaz Rossaye, Gor Mahia ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kusaka goli na katila dakika ya 59, Kiungo Deus Kaseke anafanikiwa kupata goli la kwanza akiwa anaacheza mechi yake ya kwanza tangu arejee kutoka Singida United alipodumu kwa msimu mmoja.
 Kikosi cha Yanga kilichoanza katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliomalizika kwa Gor Mahia kuondoka na ushindi wa golo 3-2 uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Kikosi cha Gor Mahia kilichoanza katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliomalizika kwa Gor Mahia kuondoka na ushindi wa golo 3-2 uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi akiondoka na mpira katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliomalizika kwa Gor Mahia kuondoka na ushindi wa golo 3-2 uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Kiungo wa Yanga Deus Kaseke akijaribu kumtoka mchezaji wa Gor Mahia katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliomalizika kwa Gor Mahia kuondoka na ushindi wa golo 3-2 uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kiungo wa Yanga Pappy Kabamba Tshishimbi akifukuzana na mchezaji wa Gor Mahia katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliomalizika kwa Gor Mahia kuondoka na ushindi wa golo 3-2 uliofanyika  Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Mashabiki wa Gor Mahia wakifuatilia mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini kilichotokea wakati wa  mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Gor Mahia uliofanyika Kwenye dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...