Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro amefanya zoezi la Ukaguzi wa malori 10 yaliyokuwa yakitokea Nchi Jirani Mara baada ya kuyatilia mashaka Kutokana na Malori hayo kudaiwa kutoka Mombasa na kupitia Njia ya Namanga tukio ambalo limeonekana sio la kawaida Kwa kupitia njia ndefu ya Mombasa kwenda Dar es salaam kupitia Namanga.

Dc Muro Akiwa katika Majukumu Yake Siku ya Jumapili Jioni alishangazwa na kitendo cha Malori hayo mapya kupita katika Wilaya yake kwa kutumia boda ya Namanga badala ya kupitia Tanga mida ya jioni yakiwa na chesses number ambazo alizitilia mashaka na kuwaagiza Maofisawa TRA kuyagua Ili kujiridhisha kwanza kutokana na kuwepo Kwa tetesi ZA baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kutaka kuhujumu Bandari Za Tanzania na Kukimbilia Nchi Jirani kutokana na Bandari Za Tanzania kuwa na Udhibiti Mzuri wa Vitendo vya Magendo na Rushwa . Dc Muro Amesema katika Wilaya Anayoiongoza ya Arumeru Kamwe haitakuwa Uchochoro wa Kupitisha Bidhaa Haramu ZA Magendo kutoka Nchi Jirani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...