Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wasanii wa kuchonga vinyago (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge jijini Dar es salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Geofrey Mngereza na kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Uchongaji, Adrian Nyangamale.
Baadhi ya wasanii wa sanaa za uchongaji wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Uchongaji, Adrian Nyangamale (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wasanii wa kuchonga vinyago (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Geofrey Mngereza. Picha na MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...