Na Mwandishi wetu
Mfanyabiashara wa Samani anayeinukia kwa kasi nchini Jacqueline Mengi amenyakua tuzo za biashara za Stevie ya Mjasiriamali wa mwaka kategori ya uzalishaji kupitia kampuni yake ya Amorette Ltd.
Katika tuzo hizo sehemu ya uzalishaji (Manufacturing), tuzo ya dhahabu ya mjasiriamali ilienda kwa watengenezaji wa lishe Hauppauge, New York Marekani na ilienda kwa Jason Provenzano, ambaye ni mwasisi na ofisa mtendaji mkuu wake.
Jacqueline Mengi atakabidhiwa tuzo hiyo Oktoba 20 mwaka huu mjini London, Uingereza.
Tuzo za dhahabu, fedha na shaba zinatolewa baada ya ushindani mkali miongoni mwa washiriki 3,900 kutoka taasisi na watu binafsi wa mataifa zaidi ya 74.
Hizi ni tuzo za kimataifa zinazotolewa katika madaraja mbalimbali ya menejimenti, kampuni, masoko, mahusiano, huduma za kijamii, ujasiriamali, utoaji wa bidhaa mpya, bidhaa mpya za tehama, tuzo kwa tovuti na zaidi.
Zaidi ya watendaji 270 duniani kote walishiriki katika kuwania tuzo hizi wakifanyiwa tathmini na majaji 12.
Jacqueline Mengi ambaye ndiye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Amorette akizungumzia ushindi wake alisema amefurahishwa na ushindi huo ikionesha kwamba mchango wake duniani unatambuliwa.
Amorette ni kampuni ya kutengeneza samani zinazotokana na mbao zinazopatikani nchini Tanzania ikiwemo miti migumu.
Samani zinazotengenezwa huangaliwa kwa undani ili kukamilisha umaridadi wa samani. Yeye pamoja na kuwa balozi wa WildAid na akiwa ndani ya bodi kadhaa; mama wa watoto pacha wavulana; mke kwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na akiendesha taasisi ya hisani ya elimu), Jacqueline huhakikisha anakagua kila samani inayozalishwa kiwandani kwake kabla ya kuuzwa au kusafirishwa.
Jacqueline, mzaliwa wa Tanzania, aliyefunzwa kubuni uzuri wa ndani, ni mwanzilishi na mbunifu mkuu wa Molocaho by Amorette, kampuni ya Tanzania inayojishughulisha na utengenezaji wa samani bora kwa namna mteja anavyohitaji, samani, nyuzi, taa, urembaji, samani za nje na kwenye bustani.
Molocaho, moja ya makampuni ya Afrika Mashariki ya samani yanayokua kwa kasi, imejipatia nafasi kubwa ya heshima kwa kuhakikisha kwamba inatumia mali ghafi na mbao njema pekee za Tanzania kutengeneza samani zenye kwenda kimataifa.
Jacqueline Mengi ni mojawapo ya watu wanaotambulika kirahisi kabisa nchini Tanzania. Mwaka 2000 alishinda taji la urembo la Miss Tanzania na kuiwakilisha Tanzania katika shindano la urimbwende la dunia (Miss World). Baada ya muda alipata heshima ya kuwa mmoja wa wanamuziki mahiri na kuweza kutoa nyimbo kadhaa zilizoshika chati Afrika Mashariki.
Pamoja na kuwa mrimbwende na mwanamuziki anasema mapenzi yake makubwa ni ubunifu wa uzuri wa ndani wa nyumba.
Kwa tuzo hiyo inadhihirisha kwamba Amorette ni chata ya kuaminika yenye mafanikio makubwa miongoni mwa watu wa daraja la juu nchini Tanzania.
Amorette, kampuni inayoshughulika na ubunifu wa masuala ya ndani ilianzisha programu ya kusimamia mafunzo kwa mafundi wa hapa Tanzania kuwafanya mafundi wa Tanzania kufikia uwezo wa kubuni na kutengeneza bidhaa zenye hadhi ya kimataifa.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...