Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia sehemu ya bidhaa zilizokuwepo kwenye moja ya mabanda ya maonesho ya Wakulima, wafugaji na wavuvi kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea katika uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere mjini Morogoro.
Na. Andrew Chimesela – Morogoro.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametaka teknolojia mpya ya Kilimo,
Ufugaji na Uvuvi inayooneshwa kipindi cha Maonesho ya maadhimisho ya Wakulima na
Wafugaji maarufu kama Nanenane iwafikie wananchi ili kuwakwamua katika dimbwi la
Umasikini.
Dkt. Jakaya Kikwete ametoa kauli hiyo Agosti 5 mwaka huu baada ya kutembelea vipando na
mabanda ya maonesho ya Wakulima, wafugaji na wavuvi kwenye maonesho ya nanenane
kanda ya Mashariki yanayoendelea katika uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere mjini Morogoro.
Dkt. Kikwete amesema pamoja na wataalamu wa Sekta ya Kilimo, ufugaji na uvuvi kujitahidi
kuvumbua teknolojia mpya katika Sekta hiyo bado teknolojia hiyo haiwafikii wananchi wa Vijijini
hivyo amewataka pamoja na kuongeza jitihada za kuvumbua muhimu elimu hiyo waipeleke kwa
wananchi ili kuondoa umaskini miongoni mwao.
“kazi kubwa imefanyika ya utafiti, viwango vimeongezeka sana vya Ubora, suala kubwa ni
namnagani uvumbuzi unaofanywa na maabara kwenye vituo vyetu namna ya kuwafikia
wakulima” alisema Dkt. Kikwete.
Aidha, Rais huyo mstaafu wa awamu ya Nne amesema ili kuondokana na umaskini kwa haraka
wataalamu lwanatakiwa kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji namna ya kulima na kufuga
kibiashara na kuondokana dhana ya kufanya kazi hizo kwa ajili ya kujikimu peke yake.
Maonesho hayo ya 25 ya nanenane kanda ya Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa
Mwl. J. K. Nyerere katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro yanajumuisha Mikoa minne ya
Pwani, Tanga, Dar es Salaam na wenyeji Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...