KAMATI viwanda ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo imetembelea kiwanda cha kutengeneza mabati cha ALAF jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo iliyohusisha wabunge pamoja na wajumbe wa kamati hiyo ya bunge ilikuwa na leongo la kuangalia utendaji kazi wa kiwanda cha Kutengeneza mabati cha ALAF pamoja na Kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakumba katika uendeshaji wa viwanda vya hapa nchinni.

Mwenyekiti wa Kamati ya viwanda ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Suleiman Ahmed Sadiq akizungumza na wabunge pamoja na wajumbe wa kamati hiyo amesema kuwa serikali inapaswa kuhakikisha kuwa umeme unakuwa wa uhakika ili kukuza viwanda hapa nchini.

Pia amesema kuwa serikali ikae na wenye viwanda vya ndani ili kuhakiki gharama za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani ili kuzuia bidhaa za enje ya nchi kuuzwa kwa gharama ya chini kuliko ya viwanda vya ndani ya nchi.

"Serikali ikae na wenye viwanda ili kuhakiki bei za uzalishaji wa bidhaa kwaajili ya kuweka bei nzuri kwa watumiaji wa bidhaa hizo za viwandani".

"Pia sisi kama wabunge tutakaa na serikali kwajiili ya kuishauri na kuieleza ni sehemu gani kunamianya ya uongezaji wa bei za bidhaa za viwandani".
Kamati hiyo ya viwanda itatembelea viwanda tisa vilivyopo hapa nchini.

Kwa upande wao kiwanda cha ALAF wameiomba serikali na shirika la Viwanda kuangalia bidhaa zenye viwango zinazoingizwa hapa nchini ili kuwa na soko linalolingana pia wameiomba serikali kuwa na umeme wa uhakika ili kukuza viwanda vya nyumbani pamoja na kukuza uzalishaji wa bidhaa za viwandani.
Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na biasharana viwanda prof. Joseph Buchweishaija akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha ALAF mara baada ya kamati ya viwanda ya bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea katika kiwanda cha ALAF jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wajumbe na wabunge wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa ALAF, Dipt Mohanty jijini Dar es Salaam leo walipotembelea kiwanda cha ALAF.
 Baadhi ya wanakamati ya viwanda wakipata maelekezo walipo tembelea kiwanda cha kutengeneza Mabati cha ALAF jijini Dar es Salaam leo. 
 Wabunge na wajumbe wa kamati ya viwanda wakiwa ndani ya kiwanda kujionea utendaji kazi wa kiwanda cha ALAF hapa nchini.
 Baadhi ya Mitambo ya kutengeneza bomba za mstatili kwaajili ya kutengenezea mageti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...