KATIBU tawala wa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma Mhe. Zahara Michuzi ametembelea katika kijiji cha Hamai na kukagua ujenzi wa zahanati ya Hamai inayojengwa na wananchi wa kijiji hicho,pia amepata fursa ya kusikiliza changamoto zao,ambapo  pia ametoa vifaa vya ujenzi na kushiriki kufanya baadhi ya kazi za ujenzi wa zahanati hiyo.

Akizungumza na Mafundi ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai, Zahara  amesema kuwa zahanati hiyo inatakiwa imalizike kwa haraka na kwa ufanisi mzuri ili kusaidia wananchi kupunguza  umbali wa kutembea kwa ajili ya kufuata huduma muhimu ya kijamii ya afya.

Pia wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa zahanati hiyo ya kijiji, Zahara ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo Mbao, misumari chokaa pamoja na vigae kuhakikisha ujenzi wa Zahanati hiyo unaisha kwa muda uliopangwa.

Wakati huo huo Zahara pia amewashukuru Wananchi waliojitokeza na kujitolea kujenga kituo hicho cha Afya, kwani maendeleo yanahitaji ushirikiano wa pamoja,Hivyo amewaomba waendelee na moyo huo huo wa kushirikiana ikiwemo pamoja na Serikali.

Katibu tawala wilaya ya Chemba mkoani Dodoma  Mh. Zahara Michuzi  akionesha baadhi ya vifaa mbalimbali vya ujenzi alivyochangia katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chemba mkoani Dodoma .
 Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akitembelea  ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chema mkoani Dododma.
 Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akisaidia kupaka rangi kwenye jengo la zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chemba mkoani Dododma, alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo.
Katibu tawala wa wilaya ya Chemba, Mh. Zahara Michuzi akizungumza na wajenzi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hamai kilichopo wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, mara baada ya kuchangia vifaa ya ujenzi pamoja na kuwaongezea wahandisi wa ujenzi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo la zahanati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...