Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuutumia Mradi wa Umwagiliaji wa Mwasubuya kubadilisha maisha ya wananchi wilayani Bariadi, kupitia kilimo cha kisasa kinachotumia zana za kisasa na kuufanya kuwa mradi wa mfano ambao watu wataenda kujifunza.
Mtaka ameyasema hayo katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 yaliyofanyika Kitaifa mkoani Simiyu na kuwashukuru viongozi wa Chama na Serikali, Watendaji, Watumishi, wafanyabiashara na wadau wengine waliofanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Amesema mradi huo wenye ekari 514 zitakazolimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa kutumia maji ya Bwawa la Mwasubuya lililoigharimu Serikali shilingi bilioni 1.24, utahusisha kilimo cha kisasa chenye kutumia zana za kisasa katika hatua zote kuanzia kuandaa shamba, kupanda, palizi na kuvuna badala ya kuhusisha zana za kilimo za mikono.
“ Nimewaambia watu wa Bariadi tunahitaji Kijiji kimoja ambacho tutabadilisha maisha ya wananchi na watu wataenda kujifunza na kuangalia transformation(mabadiliko) ya kile kijiji, lakini pia tunahitaji lile shamba lote la ekari 514 lilimwe pasipo kutumia mikono ya wanadamu kuanzia hatua za kuandaa shamba, kupanda, palizi hadi kuvuna” alisema
Ameongeza kuwa dhamira ya Mkoa ni kuona wananchi wanalima kisasa kwa kutumia zana bora za kilimo ambazo baada ya mazungumzo na Kampuni ya Agricom Africa imekubali kuikopesha Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi zana zote muhimu ili kuwawezesha wakulima katika mradi wa Mwasubuya kuongeza tija katika uzalishaji.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...