NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA 

MKUU wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,ameielekeza halmashauri ya Mafia kukaa meza moja na baadhi ya wawekezaji wilayani humo ili kuangalia namna ya kulipa kodi itakayosaidia kuondoa udumazi wa mapato kwenye halmashauri hiyo. 

Pamoja na hilo ,amewataka watanzania kuacha kuchagua kazi ,bali watumie fursa ya viwanda vingi vinavyojengwa kupata ajira .
Mkuu huyo wa mkoa huo aliyasema hayo ,wakati kamati ya siasa ya mkoa ilipokwenda kutembelea uwekezaji mkubwa wa shamba la ufugaji samaki aina ya kamba katika kiwanda cha Alpha Crust . 

Alisema ,uwekezaji huo ni mkubwa ambao umegharimu dollar za Kimarekani milioni 15 sawa na sh. bilioni 32 za Kitanzania ,hivyo ni lazima uungwe mkono kwani ni moja ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika sekta ya uvuvi . 

Aidha, aliitaka uhamiaji pamoja na idara ya kazi kuacha urasimu katika kutoa vibali vya kuishi na vya kazi kwa wataalamu mbalimbali kutoka nje ya nchi ,wanaokuja kwa ajili ya kusimamia uzalishaji katika viwanda. 

 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo (mwenye shati la kijani)akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha Alpha Crust (wa kwanza kushoto) na wa pili kutoka kulia ni Katibu tawala Mkoa wa Pwani (RAS).(Picha na Mwamvua Mwinyi) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...