Frank Mvungi- MAELEZO, Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Mhe. Adam Mgoyi  amewataka wananchi kutumia fursa zinazotokana na urasimishaji ardhi uliowezesha kutolewa kwa hati zaidi ya 300 za kimila za kumiliki ardhi kwa wakazi wa Kata ya Magubike Wilayani humo jana.
Akizungumza na mamia ya wananchi  wa Kijiji hicho waliojitokeza katika hafla ya kutolewa kwa hati hizo amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano  ni kuleta ukombozi wa kiuchumi kwa wananchi wake kupitia mpango wa matumizi bora ya adhi uliotekelezwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara  za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) na Halmashuri ya Wilaya hiyo.
“Tumieni hati hizi kutatua changamoto za kiuchumi kwani zinawawezesha kupata mitaji kutoka  katika taasisi za fedha zilizopo ambazo zimeonesha nia yakuwawezesha wananchi na nyingine zimeanza kutoa mikopo kwa wananchi wetu wenye hati za kimila” Alisisitiza Mgoyi.
Akifafanua amesema kuwa hati  hizo zitasaidia kuondoa migogoro ya ardhi, kuongeza thamani ya ardhi na kuwapa wananchi uwezo wa kujiendeleza kiuchumi ambapo tangu MKURABITA ianze zoezi la urasimishaji ardhi Wilayani humo wananchi wengi wamenufaika na mikopo iliyowawezesha kuwa na kilimo chenya tija.
Aliongeza kuwa Vijiji 37 vimenufaika na mpango wa matumizi bora ya ardhi katika Wilaya ya Kilosa ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“ Halmashuri ya Wilaya inao wajibu wa kutenga sehemu ya mapato yake ya ndani kuwawezesha wananchi katika upimaji wa ardhi na kuleta mpango bora wa matumizi ya Ardhi” Alisisitiza Mgoyi.
Pia kwa kuzingatia umuhimu wa kurasimisha ardhi Mgoya alibainisha kuwa mpango huo  unasaidia kubainisha maeneo ya ufugaji na yale ya kilimo katika Wilaya hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akisisitiza kuhusu wananchi kutumia hati  za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo ikiwemo kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha wakati wa hafla ya kuwakabidhi wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa hati hizo zilizotolewa baada ya maeneo yao kurasimishwa kwa kupimwa
 Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi. Serapia Mgembe akisisitiza umuhimu wa hati za kimila za kumiliki ardhi katika kuchochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi wakati wa hafla ya kutolewa kwa hati hizo kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani kilosa ambapo Mpango huo kwa kushirikiana na Halmashuri ya Wilaya hiyo wamefanikisha upimaji wa ardhi katika Vijiji 37.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akimkabidhi mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Magubike hati kimila ya kumiliki ardhi.
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\Magubike\2b.JPG

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Magubike wakipatiwa Hati Miliki za Kimila na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi. Pichani ni Bw. Jackson Mgoma, akiwa katika furaha baada ya kuipata Hati hiyo.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...