Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameendelea na ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Iramba kwa kutembelea bwawa la Urughu na kuwataka wakazi wa eneo hilo kusimamia rasilimali hiyo kwa mustakabali wa maisha yao ili kuendeleza fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na masuala ya uvuvi na kilimo.

Mhe. Makamba amesema ili bwawa hilo liweze kutangazwa kama eneo lindwa ki-mazingira ni lazima wananchi wawe na utashi, utayari na uwezo wa kutunza bwawa hilo kwa kufuata masharti yatakayotolewa katika tangazo la Serikali ikiwa ni miongoni mwa maeneo 77 yaliyopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira.

Waziri Makamba amesema uhifadhi wa bwawa hilo utaendana na makatazo kwa baadhi ya shughuli za kibinadamu ili kulinusuru ikiwa ni pamoja na kuzuia shughuli za uvuvi na kilimo kisicho endelevu katika Vyanzo vya maji. Aidha, Waziri Makamba ameutaka Uongozi wa Wilaya ya Singida kupitisha azimio lao la kuhifadhi bwawa la Urughu na Msitu wa Ushora katika Baraza la Madiwani.

Waziri Makamba ameahidi bila kuchelewa kutangazwa Bwawa la Urughu kuwa eneo nyeti kimazingira na kusaidia kuondoa kadhia ya kujaa kwa mchanga katika bwawa hilo. “Ili sisi tuendelee na mchakato huo tuleteeni sifa za maeneo husika kama vile, milima, mabwawa na mashamba yenye umuhimu mkubwa na historia inayojenga hoja ya umuhimu wa ulinzi katika eneo hilo, pia lipatikane azimio la Baraza la Madiwani kuwa ni eneo nyeti na kuwasilisha ombi ili Waziri aweze kuchukua nafasi yake kisheria” Makamba alibainisha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula mara baada ya kuwasili Wilayani hapo kwa ziara ya kikazi. Waziri Makamba ametembelea bwawa la Urughu na Ziwa Kitangiri ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa kuwa maeneo lindwa kimazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wakazi waishio pembezoni mwa ziwa Kitangiri Wilayani Igunga. Waziri Makamba amewaasa wakazi hao kuwa chachu katika kuhifadhi mazingira ya ziwa hilo kwa manufaa ya sasa na baadae.
Wakazi wa mwalo wa Shauri-Tanga katika Ziwa Kitangiri Wilayani Iramba, wakizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba juu ya namna wanavyotumia ziwa hilo kwa shughuli za uvuvi.

Bwawa la Urughu lilipo Wilayani Singida liko hatarini kutoweka kutokana na matumizi yasiyoendelevu ya shughuli za kibinadamu yanayopelekea kujaa mchanga na kupungua kwa kina cha maji. Waziri Makamba ameazimia kutangaza bwawa hilo kama eneo lindwa kimazingira ili kuweka ulinzi na matumizi endelevu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...