Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wanafanya
kongamano la kwanza na la kihistoria juu ya maendeleo mbalimbali
yaliyotokea katika utoaji wa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology)
barani Afrika.
Kongamano hilo la siku nne linashirikisha nchi 15 za Afrika ikiwamo Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Ivory coast, Swaziland, DRC, Madagascar, Ghana, Ethiopia pamoja na Burkinafaso
Akifungua kongamano hilo leo jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Bakari Kambi amesema azma ya serikali ni kuendelea kuboresha huduma za afya nchini ili kuwawezesha Watanzania kupata matibabu ndani ya nchi .
‘’Miongoni mwa malengo makubwa ya serikali ya awamu ya tano ni kupanua wigo wa utoaji huduma za afya kwa wananchi na kuhakikisha huduma za kibingwa na ubingwa wa juu zinatolewa hapa hapa nchini ili kuwawezesha wananchi wengi kupata huduma hizo,’’ amesema Prof. Bakari.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru amesema kukutana kwa watalaam hao ni hatua nzuri ya kuangalia namna bora ya kutoa tiba ya kisasa kwa magonjwa ya damu na hata kuanzisha tiba hiyo sehemu za kanda ili kupunguza idadi ya wagonjwa wengi ambao wanakuja kupata huduma hiyo Muhimbili.
“MHN tumekua wenyeji wa kongamano hili ambalo limehusisha wataalam wa magonjwa ya damu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, hii ni heshima kubwa na itasaidia kufikia malengo ya kutoa huduma kwa wananchi wengi zaidi,’’amesema Prof. Museru.
Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Bakari akizungumza na wataalamu wa magonjwa ya damu (Haematology) kwenye kongamano la kwanza ambalo limeandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza kwenye kongamano hilo baada ya kuwakaribisha wataalam wa magonjwa ya damu kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Wataalamu wa magonjwa ya damu kutoka nchi mbalimbali duniani wakifuatilia mkutano huo leo ambao unafanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Baadhi ya nchi zinazoshiriki kongamano hilo la siku nne ni Nigeria, Ghana, Bostwana, Afrika Kusini, Ufaransa, Marekani, Rwanda na Italia. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...