*Serikali yazindua rasmi Mfumo wa Taifa wa huduma za hali ya hewa

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SERIKALI imesema ipo haja kwa Watanzania wote nchini kuhakikisha wanajenga tabia ya kuheshimu na kuthamini taarifa za kitaaluma ambazo zinazotolewa nchini zikiwamo zinazohusu taarifa ya hali ya hewa.

Pia imesema taifa lolote linapanga mipango ya maendeleo ni lazima kuwepo na mfumo madhubuti wa kupata taarifa za hali ya hewa hasa kwa kuzingatia uwepo wa changamoto ya mbadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde aliyekuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa nchini wenye lengo la kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinafika kwa wakati na kufanyiwa kazi kikamilifu.

Uzinduzi huo umeshuhudiwa na wageni waalikwa kutoka taasisi na Wizara mbalimbali za Serikali ambapo pia Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani naye ameshuhudia tukio hilo baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Rwanda.

Akizungumzia mfumo huoMavunde amesema umekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwenye mchakato wa maendeleo ya watu na uchumi wa viwanda.Na hivyo kupata taarifa sahihi za hali ya hewa ni muhimu kwani hata unapopanga mipango ya maendeleo ni vema kujua na taarifa za hali ya hewa.
Katibu Mkuu Shirika la Hali ya Hewa Duniani Prof.Petteri Taalas ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Agnes Kijazi na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...