Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inawatafuta Zacharia Hanspope ambaye aliyekuwa mjumbe wa kamati ya Simba Sports Club na ndugu Franlin Peter Lauwo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ranky Infrastrure & Engineering iliyopewa zabuni ya kujenga uwanja wa Simba kujibu kesi ya jinai namba 214/2017. 

 Akizungumza na Waandishi wahabari jijini Dar es Salaam leo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Generali John Mbungo amesema Mshatakiwa wa kwanza Zacharia Hanspope aliondoka nchini mnamo April 8, 2018 kupitia mpaka Horohoro kwa kutumia Passport namba TA00422. 

 “Mfanyabiashara huyu aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba Sports Club na ambaye alizaliwa Iringa Mjini kabla ya kuondoka alikuwa anaishi Mlalakuwa Mikocheni ambako amebainika kuwa anamiliki hati za kusafiria tatu ambapo moja ni hati ya kusafiria ya Afrika Mashariki na hati mbili za kusafiria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotolewa kwa vipindi viwili tofauti ambapo hati ya kwanza yenye nambari AB710516 ya 16 April 2016 na nyingine ni hati yenye nambari AB 92 9732 iliyotolewa tarehe 16 Novemba 2017,” amesema 
 Amesema kuwa mshatikiwa namba moja anashtakiwa kwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kuhusiana na malipo ya kodi K/F106(1)(A)&(C) Cha kodi ya mapato chini ya sharia ya kodi namba 332.R.E 2008 kwamba kati ya washtakiwa wenzake Evans Aveva na Godfrey Nyange walitoa maelezo ya uongo kwenye ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania.
Amesema kuwa maelezo hayo yalikuwa kwamba Simba Sports Club wamenunua nyasi bandia kutoka kampuni ya Ninah Guanzhou Trading Limited kwa thamani ya Dola za Marekani 40,577.00 USD, maelezo ambayo yalikuwa ya uongo kwania nyasi hizo zilinunuliwa kwa 109,499.00 USD.

Generali Mbungo alisema Franklin Lauwo anashtakiwa kwa kosa la kufanya biashara ya ukandarasi bila ya kusajiliwa K/F22(1)(D) Cha usajili wa wakandarasi Sura ya 235 ya 2002 Kwamba kati ya Machi 2016 na Septemba 2016 Mshatakiwa alifanya kazi za ukandarasi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Simba Sports Club Uliopo Bunju Manispaa ya Kinondoni kwa thamani ya Tsh 249,929,704 wakati akiwa hajasaliwa katika bodi ya wakandarasi Tanzania hivyo kisheria alikuwa haruhusiwi kufanya kazi hiyo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Generali John Mbungo akiongea na wanahabari jijini Dar es salaam leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...