Na Heri Shaaban

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sheila Edward ,amepiga marufuku shuguli za uchimbaji mchanga na ulimaji mchicha katika bonde la mto msimbazi.

Katibu Tawala alitoa tamko hilo Dar es Saalam jana wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne shauri alipokuwa akifanya ziara ya kukagua madaraja ya Ulongoni A na B pamoja na kutembelea kukagua miradi ya DMDP.

"Kuanzia leo marufuku shughuli za uchimbaji Mchanga katika mto Msimbazi  mnasabisha maji kupoteza mwelekeo madaraja yanakwenda na maji na kuisababishia serikali hasara "alisema Sheila.Aliwataka wananchi kuacha uchimbaji mchanga katika mito yote kwani pia wanasababisha uharibifu wa mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Ilala Jumanne Mshauri alisema,daraja la Ulongoni lilijengwa mwaka jana leo (jana)ameongozana na wataalam wake kuja kuangalia athari zilizotokea katika daraja hilo na kufanya taratibu wa kujenga upya."Nimeongozana na wataalamu wangu wa Halmashauri wameona wataanda mchoro kwa ajili ya taratibu za kuanza ujenzi wake mara moja "alisema Mshauri.

Alisema dhumuni la ziara hiyo kukagua miradi yote ya serikali kuangalia inavyoendelea kujengwa ambapo pia ziara hiyo ilitembelea miradi ya DMDP ikiwemo barabara na kituo cha afya Buguruni  Mnyamani.Amewagiza maofisa Watendaji wa kata na Mtaa kuwakamata wananchi wanaotiririsha maji machafu ya (vyooni) katika mito na wale walioelekeza mabomba ya maji hayo barabarani .

Kwa upande wake Ofisa Mazingira Manispaa ya Ilala Ardom Mapunda  ametoa wito mto msimbazi kila siku unapanuka wito kwa wananchi  shughuli za uchafuzi wa mazingira Uchimbaji mchanga marufuku ukikamatwa hatua kali zitachukuliwa.
Katibu Tawala Wilaya Ilaĺa Sheiĺa Edward akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Mashauri,katika ziara ya kukagua madaraja ya Ulongoni A na Ulongoni B  Tarafa ya Ukonga wilayani Ilala,pamoja na ziara ya kukagua miradi ya DMDP (PICHA NA HERI SHAABAN)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...