Na Agness Francis,Globu ya Jamii
Kampuni
ya burudani ya Isbah entertainment imedhamiria kuwainua wasanii wa
muziki wa kiasili aina ya mnanda,vanga,mdundiko pamoja na segere ambao
wamesahaulika kwa muda mrefu.
Katika
kuwasaidia wanamuziki hao pamoja na kurejesha heshima ya muziki huo kwa
jamii, kampuni hiyo imeandaa tamasha kubwa litakalotambulika kwa jina
la Wakwetu Festival wakiwa na kauli mbiu isemayo Vumbi tu.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi zao Mratibu wa tamasha hilo Yakub
Sadik amesema kuwa lengo la kuandaa shoo hiyo ni kutaka kuwapa nguvu
wasanii waliosahaulika ili muziki huo urudi tena Kama ilivyokuwa zamani.
"Tukiwapa
njia nzuri na kuwarudisha katika gemu wanamuziki hao na wao watainuka
na kujiendeleza kama ilivyo singeli kwa sasa imepiga hatua, vile vile
pia hata makampuni mengine watahamasika kuandaa matamasha makubwa kwa
wasanii hao" amesema Yakub.
Mratibu
huyo amesema kwa sasa wataanzia katika Jiji la Dar es salaam huku
wakiendelea kujipanga kujiandaa kwenda mikoa mingine zaidi na kufika
nchini kote Tanzania.
Wasanii
watakao toa burudani siku hiyo ni Dogo Niga,Jack Simela,Mczo,Jagwa dege
la jeshi,Mzee wa bwax,Mfalme ninja,Yuda Msaliti,Ezy man,Segere,Majid
Migomba na wasanii hao watasindikizwa na wasanii wangine ambao ni Sholo
Mwamba,Manfongo,Dula Makabila pamoja na Mataluma mama mubaya.
Tamasha
hilo la aina yake linatarajia kufanyika Septemba 16 mwaka huu katika
viwanja vya Leadars Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi mpaka 12
jioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...