Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
KAMPUNI ya Vision Investments imeandaa maonesho yatakayokuwa yanafanyika nchi nzima kila mwaka ambayo yatajulikana kwa jina la Consumer Expo & Symposium.

Lengo la maonesho hayo ni kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tano chini ya uongozi wa mahiri wa Rais Dk.John Magufuli katika kuleta maendeleo ya Watanzania wote.

Kampuni hiyo imesema inatambua mkakati wa kuipeleka Tanzania katika uchumi wa viwanda na hivyo nao wameamua kuchukua jukumu hilo kwa kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kuunga mkono mkakakati huo.

Hivyo katika kuhakikisha wanafanikisha mkakati huo Kampuni hiyo imefafanua kuwa Consumer Expo ni maonesho ya bidhaa mbali mbali ambayo yalianza Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Uongozi wa kampuni hiyo umesema wanataka kuhakikisha watanzania wanajivunia na kujionea matunda ya viwanda kulingana na muamko wa viwanda vipya.

“Consumer expo inatoa fursa kwa wafanya biashara wakubwa na wadogo kutangaza bidhaa zao. Hivyo ni maonyesho yanayotoa fursa kwa washiriki kuuza na kujitangaza,”amesema.

Imeelezwa kuwa haitokuwa na tija kama viwanda vinaanzishwa lakini bidhaa hazipati kuonekana kwa walengwa kirahisi.

“Wazalishaji wengi wanaweza wasiwe na uwezo wakushiriki maonesho kutokana na gharama lakini Consumer Expo ndio tiba ya hili kwani ushiriki wake ni wa kiwango cha chini pamoja na siku zakutosha,”umefafanua uongozi wa kampuni hiyo.

Wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage ambapo pia katika maonyesho hayo yalifungamana na semina kwa muda wa siku tatu.

Semina hiyo ilijikita kuhusu jinsi yakukuza mitaji na uwekajimahesabu; umuhimu wa kuzingatia taratibu mbalimbali na viwango pamoja na masuala ya bima katika karne hii.

Imeelezwa semina hizo ni bure kwa washiriki wa Consumer Expo na wananchi kiujumla na kwamba maonesho hayo yanatoa fursa kwa wazalishaji kukutana na walaji moja kwa moja.

Maonyesho haya yanawezeshwa na NSSF, NIC, TFDA, Alliance Life Assurance, Five Star,Lake Gas, Azania Group, Sunbelt, Dabaga, Kays Hygiene, Yamoto Matches, na ,Candyman.
Ofisa Bima wa Shirika la Bima la Taifa, Rabecca Itambu,(kulia) akifafanua jambo mbele ya Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani,Dkt.John Mduma,(kushoto) wakati wa kutembelea mabanda ya maonyesho ya wajasilia mali yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Moja Jijini Dar es Salaam jana. katikati ni Mratibu wa Maonyesho, Ally Nchahaga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...