Na Karama  Kenyunko, blogu ya jamii
Kampuni zinazochezesha michezo ya kuhabatisha Nchini zimetakiwa kuhakikisha zinachezesha michezo hiyo kwa weledi na kuwapatia washindi haki zao punde tu wanapotangazwa sambamba na na kutoa elimu kwa washiriki wa michezo hiyo na kuhamasisha kucheza kwa kiasi ili kutokuwa na taifa la watu wanaojikita kucheza bahati nasibu tu kuliko kufanya kazi. 

Meneja Ukaguzi na Udhibiti wa bodi hiyo Sadicki  Elimsu ameeleza hayo leo Septemba 27.2018 alipokuwa akizindua mchezo mpya wa kubahatisha ujulikanao kwa jina la Daka wenye kauli  Mkuu ya 'Pesa Chapchap'.

Amesema kama kampuni hizo zitaendesha michezo hiyo kwa weledi basi haiwezi kuleta migogoro wala ugomvi katika jamii hasa vijana ambao ndio wanaonekana mstari wa mbele katika kucheza michezo hiyo .

" Mara zote bodi imekuwa ikisimamia michezo hii na kutoa  ushauri kwa kampuni zote zinazocheza kuchezesha michezo hiyo kwa weledi kwani pamoja na was kupata faida lakini pia michezo hii imekuwa njia moja wapo kwa vijana kupata ajira,  serikali kupata kodi na washiriki kupata fedha za kujikwamua na umaskini, " alisema. 

Kwa upande  wake, Meneja Masoko wa kampuni ya Techhub Ltd inayoendesha mchezo huyo wa Daka, Selesi  Mapunda amesema una lengo kubwa la mchezo huo ni kusaidia kubadili hali ya maisha ya wachezaji husika hasa kwa wale watakaofanikiwa kucheza na kujishindia zawadi mbali mbali zikiwemo pesa taslimu au zawadi nyingine mbali mbali.


Amesema, mchezo huu kwetu utakuwa ukiangalia washiriki wote,"wanachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi kwa kutumia simu yako kwenda namba 727272 ambapo kampuni za simu zilizopo nchini mchezaji anaweza kufanya muamala kwa kupitia kumbukumbu namba teule ambayo ni 500 au 1000,"alisema. 

Naye Balozi wa mchezo huyo,  Jacob Steven 'JB' amewataka watanzania kuhakikisha wanacheza mchezo huo kwa wingi kwani hakuna ubabaishaji wowote utakaofanywa kwa watakaobahatika kushinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...