*Waziri asema uwezo wa kivuko ilikuwa kubeba watu 101 lakini siku ya tukio kilibeba watu 265

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amesema hadi sasa idadi ya miili ya watu waliokufa kutokana na kuzama kwa kivuko cha MV.Nyerere imefikia 224.

Pia amesema uwezo wa kivuko hicho ni kubeba watu 101 lakini kimebainika kuwa watu ambao walikuwa kwenye kivuko hicho walikuwa 265 ambayo ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kivuko hicho.

Waziri Kamwelwe amesema hayo leo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa maziko ya miili tisa ambayo imezikwa na Serikali kati ya miili 224 iliyopatikana baada ya tukio hilo.Amefafanua kati ya miili hiyo 224 ambayo imepatikana wanawake ni 126,wanaume 71.Pia watoto wa kike ni 17 na watoto wa kiume ni 10

Pia amesema miili ambayo imetambuliwa ni waliotambuliwa ni 219 na wote wamechukuliwa na ndugu na miili ambayo bado haijatambuliwa ni watu wanne ambao hao watazikwa na Serikali leo.Ameongeza kuna miili ya watu watano ambayo hiyo itazikwa pamoja na miili ya watu wanne na kufanya jumla ya miili ambayo itazikwa leo ni tisa.

Waziri Kamwelwe amesema miili ambayo haijatambuliwa imechukuliwa DNA na kisha kukabidhiwa kwa ndugu au vyovyote itakavyoamriwa.

Wakati huo huo amesema kwamba baada ya kutokea kwa tukio hilo watanzania wote wamonesha ushirikiano mkubwa na kwamba michango ambayo imepatikana ni Sh.Milioni 190 na tayari wamefungua akaunti maalum ya maafa inayofahamika Mv.Nyerere.
Baadhi ya Masanduku yenye miili ya Marehemu waliofariki kufuatia kivuko  cha MV Nyerere kupinduka na kuzama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...