NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

MWILI wa marehemu Celina Sulubu, mkazi wa Lubambawe wilayani Mkuranga,mkoani Pwani umefukuliwa kwa taratibu za kisheria baada ya mumewe Selemani Hija Usumba kukiri kumuua mkewe huyo. 

Mnamo septemba 21 Usumba inadaiwa alifika kituo cha polisi Mkuranga na kuripoti kuwa mkewe Celina ametoweka nyumbani kwake tangu septemba 13 mwaka huu. 

Kamanda wa polisi ,mkoa wa kipolisi Rufiji ,Onesmo Lyanga alisema baada ya kupokea taarifa hiyo mkuu wa upelelezi wilaya ya Mkuranga alifungua jalada la uchunguzi na kumshikilia kwa mahojiano na uchunguzi zaidi . 

Alieleza ,katika mahojiano ya awali alikiri kumuua mkewe kwa kumkaba shingoni na kumsababishia kifo mkewe.Lyanga alisema ,baada ya kutenda kitendo hicho aliamua kuchimba shimo kwenye shamba la jirani ambalo alikabidhiwa kulilinda na kisha kumzika . 

"Mnamo septemba 22 timu ya makachero ikiongozwa na mkuu wa upelelezi wilaya ya Mkuranga pamoja na mashahidi mbalimbali wa tukio hili walifika eneo la tukio kwa kuongozwa na mtuhumiwa " alifafanua Lyanga. 

Lyanga alisema ,baada ya kufika eneo hilo mtuhumiwa alionyesha eneo alilozika mwili wa marehemu na kuanza kuufukua mwili huo kwa taratibu za kisheria. Kamanda huyo alibainisha ,mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi . Lyanga alisema ,chanzo cha tukio hili bado unachunguzwa. 

Aliwaonya wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani nao hawatasalimika.
Mwili wa marehemu Celina Sulubu, mkazi wa Lubambawe wilayani Mkuranga,mkoani Pwani ukifukuliwa kwa taratibu za kisheria baada ya mumewe Selemani  Usumba kukiri kumuua mkewe huyo.
(Picha na Mwamvua Mwinyi) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...