Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
RAIS
Dk.John Magufuli ameagiza flyover ya Mfugale iliyopo makutano ya Tazara
ifungwe kamera haraka ili watakaosababisha ajali wawe wanajulikana huku
akisisitiza umuhimu wa daraja hilo kutunzwa na isiwe chanzo cha ajali.
Ametoa
kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi flyover ya
Mfugale ambapo pamoja na mambo mengine amesema ni lazima kamera zifungwe
tena haraka.
Rais
Magufuli amefafanua "Nataka hapa katika flyover ya Mfugale pafungwe
kamera.Tangazenu zabuni haraka kama mtaamua kumpa aliyejenga daraja sawa
kama kumpa zawadi." Daraja hili ni la Mfugale na bahati nzuri Mhandisi
Mfugale yupo ,hivyo naamini mtalifanyia kazi haraka,"amesema Rais
Magufuli.
Amefafanua
kwamba kukiwa na kamera itakuwa rahisi hata ambaye amelewa na
akasababisha ajali na kukimbia iwe rahisi kumfahamu na ajulikane.Pia
amesema madaraja mengine makubwa na flyover ambazo zitajengwa lazima
kufungwe kamera na hiyo itasaidia kulinda miundombinu mbalimbali ya
madaraja na flyover.
Rais
Magufuli amesisitiza umuhimu wa watanzania kulinda miuondombinu hiyo na
kubwa zaidi kuhakikisha haiwi sehemu ya kusababisha ajali na kupoteza
maisha ya Watanzania.Wakati
huo huo Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Dar es Salaam kwamba
kuna mikakati mingi inaendelea ya kuhakikisha adha ya msongamano wa
magar inapungua.
Amezungumzia ujenzi wa flyover mataa ya Chang'ombe pamoja na eneo la Magereza ambapo amesema mazungumzo yalikwishaanza.Pia
amesema kuna ujenzi unaendelea eneo la mataa ya Ubungo jumla ya
sh.Bilioni 247 zitatumika kwa ajili ya eneo hilo ambapo katika eneo
hilo kutakuwa na daraja la ghorofa tatu,hivyo magari yatakuwa
yanapishana juu kwa juu.
Pia
amesema tayari ujenzi wa barabara ya mwendo kasi kutoka Mbagala hadi
Grezani mchakato wake unakwenda vizuri na itaanza kujengwa.Amesema
anataka kuipendeza Jiji la Dar es Salaam na kwamba mipango na mikakati
inakwenda vizuri huku akiwahakikishia wananchi wa Jiji hilo kwamba
atafanya ziara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...