Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akifungua mkutano wa wadau wa Mazingira Jijini Arusha. Mkutano huo umeshirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na zile zisizo za kiserikali kwa lengo la kujadili changamoto ya mimea vamizi yenye athari hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akifuatilia mawasilisho ya mimea vamizi kutoka kwa Mtaalamu wa COSTECH (hayupo pichani). Kulia ni Mhe. Nape Nnauye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maliasili.
Sehemu
ya Washiriki wa Mkutano wa wadau wa kujadili changamoto za mimea vamizi.
Mkutano umefanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha. Mstari wa mbele katika
picha ni waheshimiwa wabunge waliohudhuria.
KATIKA
jitahada za kupambana na mimea vamizi nchini ambayo kwa kiasi kikubwa ina
athari kwa uchumi wa Nchi yetu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amewakutanisha wadau kutoka sekta
mbalimbali, asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali, Wenyeviti wa Kamati za
Bunge za Ardhi na Maliasili, Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati
ya Kilimo, Mifugo na Maji ili kwa pamoja waweza kujadili namna bora ya
kupambana na mimea vamizi ambayo imetapakaa kwa kasi katika maeneo mbalimbali hapa
nchi.
“Pamoja na
kwamba viumbe vamizi wageni ni janga kwa makazi asilia ya viumbe, lakini
hatujalishughulikia kikamilifu, kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia na
kukabiliana na viumbe hivi. Kwa muktadha huo, leo tumepata fursa adimu na
adhimu kutafakari kuhusu hali ilivyo kwa sasa, changamoto zilizopo na kujadili
mikakati madhubuti ya kukabiliana na tatizo la viumbe vamizi wageni hapa nchini”
Makamba alisisitiza.
Wadau
waliohudhuria mkutano huo wameitaka Serikali kuongeza nguvu katika kupambana na
tatizo hilo kwa kuibua miradi mbalimbali kote nchini ili kwa pamoja kuwa na
mkakati wa kitaifa wa kupambana na hali hiyo ambayo ina athari kubwa kiutalii.
Mhe.
Innocent Bashungwa Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na
Mazingira amesema kuwa suala kubwa ni kuuongeza bajeti kila mwaka katika sekta
ya usimamizi wa mazingira pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Mazingira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...