NA TIGANYA VINCENT
WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wamekutana kwa ajili ya kuwaombea wananchi waliopoteza maisha yao  baada ya kuzama meli ya MV Nyerere tarehe 20 Mwezi huu katika Kisiwa cha Ukara mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa maombi hayo jana jioni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema Taifa limepoteza nguvu kazi kubwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi na kuwaacha wananchi wakiwa katika simanzi kubwa.

Alisema miongoni mwa waliofariki kuna watoto huku watu wakipoteza wenza wao na hivyo kubaki wagane na wajane na kuzifanya baadhi ya familia kuanza maisha ambayo hawakuyatarajia.

Mwanri alisema ni kipindi kigumu lakini ni vema wakamshuku Mungu na waendelee kumutegea  yeye katika kipindi hiki kwaku ndiye msaada wao wa kwanza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Igunga,John Mwaipopo,aliwapongeza wananchi kwa kuendeleza mshikamano na umoja kwa vile baadhi ya watu walitoa maneno ambayo yangeweza kuyumbisha mshikamano na umoja uliopo.

Kwa pande wa  Askofu wa Anglikana Tabora,Elias Chakupewa alisema kuwa Biblia inasema siku za kuishi mwanadamu ni miaka sabini hadi themanini na zaidi ya hapo ni tabu na mateso makubwa na kusema kuwa baadhi ya waliofariki walipaswa kufikia miaka sabini lakini hawakufika umri huo na hivyo kuacha majonzi mengi.

Aliwataka wananchi ambao bado wako hai kutumia somo hilo la ajali hiyo kujiandaa kihoro kwani hajui watakufaje na lini.

Maombi ya Mkoa wa Tabora yaliwashirikisha viongozi wa Dini zote, wanafunzi, wananchi na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za wakazi wa Tabora wakati wa maombi ya kuombea marehemu wa ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.
 Shekh wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi akiongoza dua ya kuwaombea wananchi walipoteza maisha kwenye ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao..
 Askofu wa Anglikana Tabora,Elias Chakupewa akiongoza maombi ya kuwaombea marehemu waliopoteza maisha katika ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao..

Viongozi mbalimbali mkoani Tabora wakiwa katika maombi maalumu ya kuwaombea wananchi waliopoteza maisha katika ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...