*Vingine vyaamriwa kusitisha utoaji wa mafunzo
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
VYUO Vikuu saba nchini vimezuiliwa kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika programu zote.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Charles Kihampa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi huo.

Wakati huohuo vyuo vitano vimeamriwa kusitisha utoaji wa mafunzo na kwa wanafunzi na wanaoendelea na masomo kuhamishwa mara moja.

Pia vyuo vingine viwili vimeamriwa kuwahamisha wanafunzi wote wanaoendelea na masomo kwani tume hiyo imefuta vibali vya vyuo hivyo.

Akifafanua zaidi Kihampa amesema Vyuo hivyo saba ambavyo vimezuiliwa kudahili wanafunzi wapya ni pamoja na Chuo kikuu cha Kimataifa cha kampala nchini Tanzania (KIUT), Chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo kikuu kishiriki cha Marian (MARUCO), Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Kadinali lugambwa CARUMUCo na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKUMU).

Pia Chuo kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania kituo cha Mt. Marko (SJUT- St. Mark's c3ntre ) na Chuo kikuu cha umoja wa Afrika Tanzania (UAUT) . 

Wakati vyuo vilivyoamriwa kusitisha utoaji mafunzo na kuamriwa kuhamisha wanafunzi wote ni pamoja na Chuo Kikuu cha Mlima Meru (MMU),Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB), Chuo Kikuu cha ECkernforde Tanga (ETU), 

Chuo kikuu cha kilimo cha na Teknologia cha Jomo Kenyatta-Kituo cha Arusha (JKUAT) Kituo cha Arusha na Chuo kikuu Kishiriki cha Josiah Kabira. (JOKUCo).

Kihampa amesema kuwa baadhi ya vyuo vipo katika uangalizi wa Tume ya vyuo kikuu Tanzania na vinaendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo hawaruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazo zote za masomo kuanzia Astashahada, Stashahada, Shahada, Shahada ya Uzamili, hadi shahada ya Uzamivu kwa programu zote mpaka vitakapoamriwa.

Pia tume ya vyuo vikuu Tanzania imevitaka vyuo vyote kuzingatia na kutekeleza maagizo waliyopewa na inawaarifu wanafunzi wote wanaotakiwa kuhama kuwasiliana na vyuo vyao kwaajili ya maelekezo kuhusu kuhama na vyuo wanavyotakiwa kuhamia.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Bodi ya Mikopo Tanzania Deus Changala amesema kwa wanafunzi waliokuwa na mikopo katika vyuo hivyo wasiwe na wasiwasi mikopo yao wataendelea kuipata wakati wakiwa kwenye vyuo watakavyohamia.
Mtendaji wa Mkuu wa Tume ya Vyuo vikuu Tanzania Charles Kihampaakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kusitisha utoaji wa mafunzo katika vyuo mbalimbali pamoja na kuamru wanafunzi wanaoendelea na masomo kuhamishwa katika vyuo vyao na kuhamia vyuo vingine.Kushoto ni Mwakilishi wa bodi ya mikopo, Deus Changala.
Mtendaji wa Mkuu wa Tume ya Vyuo vikuu Tanzania Charles Kihampaakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...