NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

BAADHI ya wakazi wa mitaa ya Lumumba ,Muheza na Kidimu (LUMUKI) wilayani Kibaha ,mkoani Pwani ,wanahitaji serikali iwasaidie kuwajengea daraja ama kivuko kwenye mto Mpiji ili kunusuru maisha yao. Wakazi hao kwasasa wanapata shida ya kuvuka kwenda mtaa wa Kibwegere kata ya Kibamba ,wilaya ya Ubungo ambako ndipo wanategemea kupata huduma za kijamii. 

Walifikisha kero hiyo ,walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi la ujenzi wa nguzo kwa ajili ya kuvusha watu . Mwenyekiti wa ujenzi wa daraja hilo la LUMUKI, Iddi Chamale alisema ,changamoto kwenye eneo hilo ni kubwa .

Aidha , wamekuwa wakiweka vivuko vya muda ambapo huweka mabanzi kwa ajili ya kuvuka ambapo wakati wa mvua kubwa yanasombwa na maji hayo. “Kivuko kikisombwa shida ndipo zinapoanza kwani hubidi watu wavushwe kwa kubebwa ambako kuna mamba wengi na ni hatari kwani maji yakiwazidia ni hatari watu wanapoteza maisha,” alifafanua Chamale. 

“Makao makuu ya wilaya ya Kibaha ni mbali lakini kwa kuvuka mto ni karibu hivyo inatubidi twende Kibwegere, tumetenganishwa na mto Mpiji lakini kinachotusumbua ni sehemu ya kuvuka ” alisema Chamale.

Nae Neema Zawadi alisema , kipindi cha mvua ni taabu kwani mawasiliano hukatika na watu hupoteza maisha wanapojaribu kuvuka huku wajawazito hujifungulia njiani kabla ya kuvuka mto. “Wanafunzi hushindwa kwenda shule wazazi huogopa wasivushwe,wafanyakazi huwabidi wakae ngambo hivyo kutorudi nyumbani hivyo hata ndoa zetu zinayumba”alisema Neema. 
 
Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Pangani iliko mitaa hiyo Agustino Mdachi ,alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema jitihada wanazofanya ni kujenga vivuko lakini havidumu . Alielezea, amekuwa akiwasilisha changamoto hiyo halmashauri lakini tatizo ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kujenga daraja. Mdachi alisema atawasiliana na wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili walishughulikie suala hilo. 

Diwani wa kata ya Pangani Kibaha mkoani Pwani, akielezea kero ya kivuko kwa wakazi wa eneo la Lumumba na Kidimu. Picha na Mwamvua Mwinyi 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...