Wateja wa Jumia kulipia bidhaa kwa Masterpass
Kurudishiwa 10% ya kiasi cha pesa watakacholipia bidhaa walizoziagiza.

Ni salama, rahisi na salama zaidi ambapo wateja hawatakiwi kulipia kwa pesa taslimu.

Dar es Salaam: Septemba 25, 2018. Katika jitihada za kurahisisha huduma za manunuzi ya bidhaa kwa njia ya mtandao nchini, Jumia imewawezesha wateja wake kulipia bidhaa zozote watakazonunua kwenye mtandao wake kwa kutumia huduma ya Masterpass.

Maboresho haya ya kufanya malipo yamekuja ikiwa ni njia ya kuwarahisishia wateja kuwa na machaguo salama, rahisi na haraka zaidi kulipia bidhaa zao. Lengo la Jumia ni kuhakikisha Watanzania wanafanya huduma zao kwa kidigitali ili kurahisisha maisha yao ya kila siku. Na huduma ya Masterpass ambayo haimuhitaji mteja kubeba kiwango cha fedha ni suluhisho tosha kwa nyakati hizi za maendeleo ya sekta ya fedha kidigitali.

Akizungumzia juu ya huduma hii mpya ya njia ya malipo ambayo imetambulishwa na Jumia, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bw. Albany James amebainisha kuwa, “huu ni mwendelezo wa Jumia katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanaweza kufanya manunuzi kwa usalama na urahisi mahali popote walipo. Kabla ya kuja na njia hii mpya ya malipo kwa kutumia huduma ya Masterpass, wateja wanalipia kwa Tigo Pesa au pesa taslimu. Tunaamini njia hii imekuja kufanya mapinduzi kwa wateja ambao wanakwenda na wakati kwa kuhifadhi fedha zao kidigitali.”

“Sio kila mtu anapenda kutembea na pesa taslimu siku za hivi karibuni. Ukiachana na sababu za kiusalama kwa wateja kutembea na kiwango kikubwa au kwa wafanyakazi wetu ambao hupokea malipo hayo kwa niaba ya kampuni, lakini njia hii mpya hurahisisha mchakato mzima. Hii ina maana kwamba badala ya mteja kutoa pesa, mteja atatumia simu yake ya mkononi kufanya malipo kwa ‘QR Code’ ya Jumia ndani ya muda mfupi tu!” alifafanua zaidi Bw. James.

Huduma hii mpya ya njia ya malipo imekuja wakati ambapo Jumia inaendesha kampeni ya ‘Electroshock.’ Kampeni hii ni ya kipekee ambayo inatoa fursa kwa wateja kununua bidhaa mbalimbali za vifaa vya umeme kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ofisini, shuleni, na binafsi. Lakini pia wateja wanapatiwa vocha za punguzo la bei mpaka shilingi 50,000 pamoja na ofa ya kupelekewa bidhaa zao mpaka mahali walipo kwa zitakazozidi shilingi 200,000 na kuendelea kwa jijini Dar es Salaam pekee!



“Jumia imekuja kufanya mapinduzi katika namna ambayo Watanzania wanafanya manunuzi yao ya kila siku. Kwa miaka mingi wamekuwa wakipoteza muda na gharama kwenda na kurudi madukani kufuata bidhaa, muda ambao ungepaswa kuelekezwa katika shughuli zingine za maendeleo. Katika kulipatia ufumbuzi suala hili, sisi tumekuja na suluhisho kwa kuyakusanya maduka yote na kuyaweka sehemu moja mtandaoni. Hii inamrahisishia mteja kuweza kuperuzi bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara tofauti ndani ya wakati mmoja mahali na muda wowote alipo na kisha kufanya manunuzi na kupelekewa bidhaa zake mpaka pale alipo. Kwa mfano, wakati huu wa kampeni ya ‘Electroshock’ mteja anaweza kuperuzi bidhaa zaidi ya 1000 za vifaa vya umeme,” alihitimisha Meneja Masoko wa Jumia Tanzania.

Katika kunogesha kampeni ya ‘Electroshock‘ ambayo inatarajiwa kufika kikomo Oktoba 7, Jumia imewapatia Watanzania ambao ni wapenzi wa mchezo ‘Playstation’ kununua bidhaa mpya ya ‘FIFA19’ ambayo haijaingia sokoni bado ikitarajiwa kuzinduliwa mnamo Septemba 28 duniani kote. Kupitia mtandao wa Jumia wateja wanaweza kuweka oda ya bidhaa hiyo na kuwa wa kwanza kuimiliki mara tu ikiingia sokoni. Lakini kama hiyo haitoshi kuna simu za bure ambazo zitakuwa zinashindaniwa kwenye mtandao huu kwa kupitia programu yao ya simu ya ‘Jumia App.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...