Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi na watumishi
mbalimbali wa wizara yake wafanye kazi kwa kushirikiana na kuacha tabia ya kunyanyasana
wakati wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.
Lugola pia amesema kila mtumishi wa wizara yake ana umuhimu mkubwa kwa kufanikisha
mafanikio ya wizara hiyo kwakuwa watumishi hao wanafanya kazi kwa kutegemeana.
Akizungumza na watumishi wa makao makuu wa wizara hiyo katika ukumbi wa mikutano wa
Chuo cha Veta, jijini Dodoma jana, Lugola alisema kikao hicho alikiitisha kwa lengo la kujuana
na watumishi hao pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi.
“Mambo muhimu ambayo yatatuletea mafanikio ndani ya wizara yetu ni kufanya kazi kwa bidii,
kufanya kazi kwa kushirikiana na tukifanya hivyo hakika tutapendana na kuzidi kufanikiwa,”
alisema Lugola.
Lugola aliongeza kuwa, hapendi kuona mtumishi yeyote ananyanyaswa kwa kutopewa haki zake
au kucheleweshewa pasipo kuwa na sababu za msingi ikiwemo malipo mbalimbali ya watumishi
wanayodai, na endapo yatatokea hayo watumishi hao wamletee kero zinazowakabili ofisini
kwake na kwa kushirikiana na katibu mkuu wa wizara hiyo watazitatua.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na watumishi wa
Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi. Pia Lugola
aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kuwataka baadhi ya
viongozi wa wizara hiyo kuacha tabia ya kuwanyanyasa watumishi wao.
Lugola alikutana na watumishi hao katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha
Veta, jijini Dodoma, leo jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu alipokua anawasili katika
ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Veta, jijini Dodoma kwa ajili ya
kuzungumza na watumishi wa wizara hiyo, leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu,
Ramadhan Kailima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...