Serikali imetaka wazazi,walimu
wakuu,watendaji wa kata na vijiji pamoja wale wote watakaousika na
vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto au kumpa mimba
mwanafunzi kuwajibiswa kwa kusababisha watoto wa kike kushindwa kumaliza
masomo yao na kusababisha wasichana walio mashuleni kushindwa kutimiza
ndoto
zao.
Hayo yalisemwa jana na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine
Ndugulile alipofanya ziara Mkoani Morogoro kupata taarifa ya Mkoa huo
kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa masuala Afya na
Maendeleo ya Jamii Mkoani humo.
Akizungumzia hali hiyo Naibu
Waziri Ndugulile alisema kiwango cha matukio haya ni kikubwa mno na
kuagiza Mkoa huo kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama ya Wanawake na
Watoto pamoja na vituo vya mkono kwa mkono (One Stop Centres) akisistiza
kuwa haya ni maagizo ya serikali kama sehemu muhimu ya kupambana na
vitendo vya ukatili nchini.
“Vituo hivi kwa nchi nzima ni
kumi kwa hiyo akikisheni mnaanzisha Vituo hivi katika Mkoa wa Morogoro
kwa kuwa ili ni agizo la serikali katika kuakikisha tunatokomeza vitendo
vya ukatili”. Aliongeza Dkt.Ndugulile.
Akisoma taarifa ya Mkoa huo kwa
Naibu Waziri Ndugulile, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jacob
alisema kuwa mkoa wa Morogoro una jumla ya matukio 2,555 ya mimba za
utotoni akiyataja matukio 1,160 kuripotiwa kutoka Dawati la Polisi
mengineyo 895 kulipotiwa katika vituo vya Afya, mashuleni na jamii.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na viongozi wa mkoa wa Morogoro na baadhi ya watumishi wa Mkoa huo hawako pichani kuhusu madhumni ya kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo pia kupokea taarifa ya masuala ya Afya na Maendeleo ya Jamii ya Mkoa jana huo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa ufafanuzi wa hali ya maendeleo sekta Afya na Maendeleo ya Jamii ya Mkoa wa Morogoro kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kabla ya Waziri huyo kuanza ziara ya siku tatu Mkoani humo .
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jackob akitoa taarifa ya Mkoa wa Morogoro kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotombelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kupata taarifa ya Mkoa huo kabla ya kuanza ziara yake ya siku tatu Mkoani humo.
Baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Morogoro wakifuatilia kwa makini maelezo na maagizo ya Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kabla ya kuanza ziara ya siku tatu Mkoani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...