Na Ripota Wetu,Kibaha

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ametembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) katika Maonesho ya wiki ya

Viwanda Mkoa wa Pwani ambapo ameipongeza TIC kwa jitihada zake katika kukuza na kuvutia uwekezaji nchini na namna inavyowahudumia wawekezaji kupitia huduma za mahala pamoja zinazotolewa na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya ofis za kituo hicho.

Akizungumza leo akiwa kwenye banda la TIC, Mhandisi Ndikilo amesisitiza ni ukweli kwamba Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa inayopokea wawekezaji wengi na hivyo nguvu ya

kuwahudumia lazima iimarishwe. Aidha ameshauri TIC kuhakikisha inapata taarifa zote muhimu zinazohusiana na uwekezaji ndani ya mkoa wa Pwani kwa kuwasilian na ofisi za Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kwani kwa kufanya hivyo kutarahisisha uratibu na huduma kwa wawekezaji nchini.

Baadhi ya tarifa alizosisitiza TIC iwe nazo ni pamoja na maeneo ya uwekezaji yaliyotyengwa, takwimu za miradi ya uwekezaji. Katika kuhakikisha kwamba Mkoa wa Pwani unaendelea kuvutia uwekezaji Mkuu wa Mkoa atawasilisha TIC maeneo ambayo tayari yametengwa kwa ajili ya uwekezaji ili yaweze kutafutiwa wawekezaji.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika banda la TIC kwenye maonesho ya Wiki ya Viwanda Mkoa wa Pwani yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo Picha ya Ndege wilayani Kibaha mkoani Pwani, Meneja wa Kanda ya Mashariki Venance Mashiba .Amesema kuwa katika kuharakisha utatuzi wa changamoto zinazowakabili wawekezaji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kimeunda Kamati Maalum ya kiaifa inayojumuisha Wakuu wa Taasisi za Serikali ambazo ni wadau katika kuhudumia uwekezaji. 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Kanda ya Pwani Venance Mashiba leo kwenye Maonesho ya viwanda mkoani humo.

 Baadhi ya wadau wa masuala ya viwanda wakiwa kwenye banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wakipata maelezo leo baada ya kutembelea maonesho ya viwanda mkoani Pwani
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisaini kitabu cha wageni leo baada ya kufika kwenye banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC). Anayeshuhudia ni Meneja wa TIC Kanda ya Mashariki Venance Mashiba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...