Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
WAFANYAKAZI watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais -Muungano na Mazingira Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa mazingira.
Wakili wa Serikali Faraja Nguka amewasomea washtakiwa makosa yao leo Oktoba 31, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando.Wakili Nguka amedai washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, mawili ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 160 milioni.
Aidha Mahakama imetoa hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa Magori Wambura (38) mkazi wa Bombambili kwa sababu wakati washtakiwa hao wakisomewa mashtaka hayo yanayowakabili mshtakiwa huyo ambae ni Ofisa mazingira wa Nemc, hakuwepo mahakani.Wakili Nguka amewataja washtakiwa hao kuwa ni Ofisa wa Mazingira NEMC Deusdith Katwale, Msewe, Luciana Lawi, Edna Lutanjuka, Ofisia Mwaruka na Lilian Laizer.Imedaiwa kati ya Septemba 27, 2016 na April I mwaka huu wa 2018 washtakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kughushi.
Katika shtaka la pili washtakiwa hao wanadaiwa, Oktoba 17,2017 kwa udanganyifu walighushi cheti cha tathmini ya uharibifu wa mazingira chenye namba ya usajili EC/EIA/3366 wakijaribu kuonesha kuwa cheti hicho ni halali na kwamba kimetolewa na NEMC wakati wakijua si kweli.Pia washtakiwa hao wanadaiwa kughushi saini ya Januari Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais -Muungano na Mazingira katika cheti cha tathmini ya uharibifu wa Mazingira chenye usajili namba EC/ EIA/3366 wakijaribu kuonesha kuwa cheti hicho ni halali na kwamba kimetolewa na NEMC wakati wakati wakijua si kweli.

WAFANYAKAZI
watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
wakiwa wamefishwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakikabiliwa na
mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais -Muungano na Mazingira Januari Makamba
katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa mazingira.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...