Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja mwaka 2018 uongozi wa bima ya afya Mkoa wa Kagera(NHIF) wameahadhimisha wiki hii kwa kwa kutoa msaada wa mashuka 60 yenye thamani ya shilingi 720,000 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Bukoba.

Meneja wa mfuko wa bima ya afya (NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo amesema wiki hii wameitumia kuwa karibu na wanachama wao kwa kutembelea vituo vya tiba na kupata maoni kutoka kwa wanachama wao.

"Tumetumia wiki hii kutembelea vituo mbalimbali vya kutolea huduma na kushuhudia upatikanaji wa huduma kwa wanachama wetu na kupata maoni yao, katika kuwa karibu na wanachama wetu kwa wiki hii mrejesho tumeupata toka kwa wanachama wetu unaonyesha wanachama wetu wamekuwa wakipata huduma nzuri na bora"alisema Odhiambo

Odhiambo aliishukuru serekali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kusimamia nidhamu kwa watumishi pamoja na kuondoa tatizo la uhaba wa dawa na vitendanishi kwani hivi sasa vituo vingi vina dawa za kutosha.

Meneja huyo pia amehaidi kuyafanyia kazi maoninyote yaliyotolewa na wanachama wa mfuko huo kwa kushirikiana na watoa huduma.Maofisa wa hao wa mfuko wametembelea vituo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa pamoja na Bukoba town Health.mwingine,Odhiambo amehadi kuyafanyia kazi kwa haraka maoni yaliyotolewa na wanachama kwa kushirikiana na watoa huduma.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera Dkt John Mwombeki ameshukuru mfuko wa bima ya afya (NHIF) kwa msaada kwakuwa utasaidia kuboresha huduma kwa wagonjwa wanaolazwa hapo.Alisema hospitali inafanya jitihada mbali mbali za kutatua changamoto ya muda wa upatikani wa huduma ikiwa ni pamoja na kuajiri madaktari wa muda.
Meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera akiongea na wagonjwa waliolazwa katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera katika wiki ya maadhimisho ya huduma kwa wateja 
Meneja wa NHIF Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea na wanachama wa mfuko huo waliofika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwaajili ya kupata matibabu.
Uongozi wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Kagera wakikabidhi mashuka 60 kwa uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya huduma kwa wateja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...